LIVE STREAM ADS

Header Ads

FAMILIA YA BINAGI ILIYOKO TARIME MKOANI MARA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO.

Familia ya Binagi ya Kijiji cha Kenyamanyori, Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara, inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Chacha Marwa Binagi (Chacha Monene), aliefariki dunia Desemba 11.2015 baada ya kuugua kwa muda.
Mazishi yalifanyika jana Desemba 14,2015 nyumbani kwake Kenyamanyori. Marehemu alizaliwa mwaka 1958 hivyo hadi mauti yanamkuta alikuwa na umri wa miaka 57. 
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.
Ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu ukipelekwa malaloni kwa ajili ya mazishi
Mtoto wa Marehemu akilia kwa uchungu
Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Starehe na Maafa akisoma Risala ya Marehemu
Mwenye kinasa sauti ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chira akizungumza katika msiba huo
Msemaji wa Familia akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki na mazishi hayo
Baba mdogo wa marehemu (wa pili kushoto) akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika Mazishi
Wazazi na wanafamilia wakiwa katika huzuni
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe, Ameni!
Zaidi BONYEZA HUKU

No comments:

Powered by Blogger.