LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI YA KAHAMA KUFUTA OFA ZAIDI YA 52 ZA VIWANJA.

Na:Shaban Njia
HALMASHAURI ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga kupitia idara ya ardhi imepanga kufuta zaidi ya ofa 52 za Viwanja Vilivyopo Mjini hapa,ambavyo viligawanywa kwa Viongozi wa Serikali ya Wilaya pamoja na Madiwani waliokuwepo katika kipindi cha nyuma kinyume cha utaratibu na Sheria za ardhi.

Akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa Halmashairi ya Mji wa Kahama Abel Shija alisema kuwa maeneo yaliainishwa kufutwa kwa ofa za Viwanja ni pamoja na eneo la kata ya Nyahanga ambapo kuna eneo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari  na kupewa mwarabu aliyenga maghala.

Alisema kuwa maeneo mengine yaliobainika kuwa hayamilikiwi kihalali ni eneo Kata ya Malunga katika Mtaa wa Igomemelo ambalo lilikuwa ni eneo lilitengwa kwa shughuli za kijamii kama vile Hospitali, Kituo cha Polisi, Nyumba za Ibada pamoja na soko ambalo pia limevamiwa na watumishi hao wa Halmashauri pamoja na Madiwani na kujengwa nyumba za makazi ya kuishi.

Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa katika ziara ya kukagua maeneo hayo ambayo yalikuwa yametolewa ofa kinyume na taratibu pia aliongeza kuwa idadi hiyo ya ofa inaweza kuongezeka kwa kuwa kuna baadhi ya maafisa ardhi katika Halmashauri ya Mji bado hawajasalimisha ofa hizo katika ofisi yake.

Aliendelea kusema kuwa katika eneo la Nyasubi kuna baadhi ya wafanyabiashara wamevamia eneo lililokuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na hivyo kupewa  mfanyabisha mmoja mmoja anayefanya shughuli za uoshaji wa magari katika eneo hilo ambalo pia likiwa halina huduma ya chaoo kwa ajili ya wafanyakazi.

Aidha shija alisema kuwa katika eneo la Kata ya Busoka nje kidogo ya Mji wa Kahama ambapo kuna shughuli za upimaji wa viwanja unaendelea alisema kuwa baadhi ya maafisa ardhi katika Halmashauri hiyo wamekuwa wakiwadhulumu Wananchi maeneo yao pindi wakipima na kuna kuna eneo kubwa limepatikana.

“Ninawaambia waandishi wa Habari kuwa nilifanya mkutano juzi na Wananchi wa kata ya Busoka na kunieleza kuwa baadhi ya Wapimaji wa viwanja kutoka katika Halmashauri yao kwa kipindi cha nyuma walidiriki kupima hadi katika maenei ya hifadhi ya barabara kuu iendayo katika nchi jirani za Burundi na Rwanda”,Alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa Halmsahuri ya Wilaya ya Kahma imejipanga kukaa kikao na Watendaji wa idara za ardhi ili kuona ni sehemu gani wamekuwa wakikosea katika upimaji wa ardhi kwani malalamiko ni mengi ya kuishutumu idara hiyo ya ardhi ya Halmashauri ya Mji wa Kahama.

“Tumepanga kukaa kikao na maafisa wangu wa ardhi ili kuona juu ya kutatua matatizo haya ya ardhi kwani malalamiko ni mengi huku hadi Wananchi wakidiriki kutotoa ushirikiano katika kupima maeneo yao kama baadhi ya maafisa wa ardhi wa Halmashauri hiyo watajumuishwa katika zoezi hilo

No comments:

Powered by Blogger.