LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAAMUZI MABOVU NA UTENDAJI MBAYA WA KAZI WAWAPELEKEA WENYEKITI KUMCHUKULIA HATUA MWENYEKITI WAO WA KIJIJI.

Wanafunzi katika shule ya msingi Shenda wakiwa wamekaa kwenye moja ya darasa lililosakafiwa
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na kilio toka kwa wananchi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na viongozi waliowachagua pasipo kuchukua hatua zozote. Ukimya huu wa wananchi ndio unaosababisha kilio hicho kuendelea kukuwa kila siku.   Ila vilio hivi huishaga pale tu wananchi wanapoamua kwa dhati kuchukua hatua, kama walivyofanya wananchi wa kijiji cha Shenda.  Shenda ni moja kati ya vijiji zaidi ya 200 vinavyofanya kazi na programu ya Chukua Hatua mkoani Geita.

Kijiji hiki kinapatikana kata ya Masumbwe wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita. Jumla ya wakazi 2,454 wanaishi katika kijiji hiki wakijishughulisha na shughuli za kilimo, uchuuzi na uchimbaji wa madini. Fredson Yaida ni mmoja kati ya waraghabishi wanaofanya kazi na program hii, kama walivyo waraghabishi wengine yeye pia alichaguliwa na wananchi na baadaye kuhudhuria mafunzo maalumu ya uraghabishi, “Baada ya kuchaguliwa basi tulienda kwenye mafunzo kule Ushirombo. Kule tulijifunza na kujengewa uwezo wa kufahamu mapato nmatumizi, kujua vyanzo vya mapato vya maeneo tunayotoka, haki na wajibu wetu katika kusimamia mali za umma lakini pia kuweza kuzihojia pale inapohitajika,” anaelezea Fredson Yaida.  Kwa kuwa mraghabishi hana mamlaka ya kisheria ya kuitisha mikutano kwa ajili ya kuwashirikisha wananchi wote kile alichojifunza, badala yake amekuwa akitembelea vikundi mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji na kushirikishana. Vikundi hivyo ni pamoja na Mkombozi, Jiandae na Twende na Wakati; kila kikundi kina wastani wa wanachama 25 mpaka 30.  

Akimuelezea jinsi anavyomuelewa mraghabishi, mwenyekiti mpya wa kijiji cha Shinde, Andrea Lubango anasema, “huyu bwana Fredson Yaida na kikundi chake wamekuwa mstari wa mbele katika ku- hamasisha wanakijiji kujua mambo ya mapato ya kijiji chao na kuwataka kuulizia ili kusudi waelewe zaidi.”   Wakati wa majadiliano na wanachama wa vikundi hivyo na makundi mbalimbali ya jamii, suala lililojitokeza ni la mapato yanayotokana na malori yanayobeba mchanga wenye masalio ya dhahabu toka kijijini hapo. Akielezea jinsi alivyoitoa hoja hiyo kwa wenzake Mraghabishi Fredson anasema,  “Niliwaambia jamani sasa hivi tuelimike sasa si mnaona magari hapa yanapakia mizigo, ushuru hatuupati, hata mapato hatusomewi imekuwaje nchi yetu hivi na tuna rasilimali na magari kila siku yanapakia mizigo, yapo magodown mengi tu yamejengwa hapa Shenda tulikuw hatupati hata shilingi.”  Malori hayo huja kubeba mchanga unaokuwa umebakia kutoka mgodi wa Shenda kwenye mawe yaliyovunjwa na wenye makarasha. Mwenye lori huja kununua mchanga huo uliobakia na kuondoka nao pasipo kijiji kupata mapato tokana na mchanga mali huo.

Mgodi wa shenda hutegemewa kama njia ya kujipatia kipato hususani wakati wa hali mbaya ya kilimo baadhi ya wanavijiji huenda kuajiriwa na wamiliki wa mashimo hayo ya dhahabu. Wanakijiji huchimba udongo kisha huchekecha ili kupata dhahabu na baada ya kuchekecha mchanga huukusanya pembeni mwa mashimo ya dhahabu kwa ajili ya kuuza. Fredson anasema wengi wa vijana ndio hujishughulisha na shughuli za migodi ili kujipatia kipato. Fununu za kuwepo kwa  wawekezaji katika mgodi wa Shenda wakawa wanajiuliza haya malori yanayopishana na shehena ya mchanga uliochanganyikana na dhahabu pasipo wao kupatiwa taarifa yoyote uliwapa shaka na hivyo kutaka kujua zaidi. Kupitia mraghabishi, vikundi na wanakijiji ukawekwa mkakati wa jinsi ya kufuatilia hivyo kupitia uhamashaji wananchi wakaanza kuongea kichinichini hatimaye wakaamua kuchukua hatua.
 Mraghabishi Fredson Yaida (wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa wanachama wa vikundi, Mwenyekiti wa kijiji (wa kwanza kulia) na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Shinde wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ofisi ya kijiji.
“Tukaanza kuhojiana sisi kwa sisi vipi mbona magari yanasomba tu, watu wakasema tuyasimamishe yasisombe, bahati nzuri serikali ya kijiji ikaliona hilo kwa haraka, wakawa wameitana mwenyekiti wa kijiji na wajumbe na mtendaji wa serikali ya kijiji. Wakaliwekea mkakati wa kulifuatilia,” anaelezea Fredson Yaida.  Kamati ya serikali ikiwa tayari imeshanusa kilichopo mbele yao iliwalazimu kuchukua hatua za haraka kujinusuru na hasira za wananchi, kama anavyoelezea mjumbe wa kamati ya kijiji, Makemba Kubezia,“Tukaanza kujiuliza sisi wenyewe wa kamati ya kijiji, mh, mbona huu mchanga unatoka kwenye mashimo yetu pasipo sisi kujua, labda hapo mwenyekiti amefanya bila kutuhusisha serikali ya kijiji. Baadaye basi katika ufuatiliaji wananchi wakaanza  kutuhoji ikabidi tuamke kweli na kuchukua Hatua stahili,”

Hivyo kamati ya serikali ya kijiji ikabidi imwite mwenyekiti wa kijiji ili kujua nini kinaendelea katika shughuli hiyo na kukubaliana kulifuatilia suala hilo ofisi ya kata na baadaye kwenda kwa mhusika  (mwenye malori) ili kujua anasomba mchanga kwa kibali kipi. Lakini katika hali ya kushangaza aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Shenda John Mapoli aliwachenga wenzake na kwenda peke yake kuonana na mtu anayeleta malori kijijini kuchota mchanga wenye masalio ya dhahabu. Baada ya kurudi hakuwaita wenzake wa serikali ya kijiji kuwapa mrejesho wa safari yake.  Kukawa na maneno ya kichini chini kwamba mnunuzi humpa mwenyekiti bakshishi (rushwa) ili apate nafuu katika bishara yake ikiwa ni pamoja na kukwepa hiyo tozo. 

Iligundulika baadae kuwa hakutaka wagundue kuwa alikuwa akipokea pesa kutoka kwa mnunuzi, kwani alikuwa hazifikishi katika ofisi yakijiji.Kutokana na kile kilichojitokeza ikabidi uitishwe mkutano mkuu wa kijiji uliosimamiwa na mtendaji wa kata. Ni dhahiri wananchi hawakuwa na imani na Mwenyekiti wao tena na hivyo kumtaka aachie madaraka na kisha kumteua mwenyekiti wa muda, Andrea Lubango atakaye kaimu kiti hicho mpaka uchaguzi ujao.  “Hivyo baada ya wananchi kumuondoa tukambana na yule mwenye lori. Kwa kuanzia akatoa kiasi cha shilingi  laki tano na miifuko 60 ya sementi kati ya hiyo, 30 imetumika kwa ajili ya ukarabati madarasa mawili na mi-fuko mingine 30 itatumika kwenye ujenzi wa zahanati, na kuna mtu  kuwalazimisha. Tatizo ni watendaji wa vijiji,”  Akitoa mfano wa hali hiyo ya watendaji wa vijiji Diwani wa kata ya Kishapu anasema,  “Kijiji hiki hapa (Kishapu) kimemaliza karibu miezi tisa bila kusoma mapato na matumizi na nimekuwa nikimtumia mtendaji wangu wa kata kwamba waandikie wawe wanasoma mapato na matumizi. Lakini na yenyewe ikawa bla bla, mpaka nikalazimika kufika ofisi ya mkurugenzi badala yake akaandikiwa, ndio akasoma mapato na matumizi,”   

Kwa upande wa Kata ya Mwakipoya mheshimwa Thabita anasema, “Watendaji wangu sio wazuri hawataki kualika mikutano, mambo yote yamekwama kwa ajili ya watendaji. Nimefanya mikutano miwilitu katika kijiji cha Mwangongo na hapa Mwakipoya. Changamoto kubwa ambayo alikumbabana nayo kwenye vile vijiji sana sana ni malalamiko kwa watendaji kwamba hawataki kusoma taarifa za mapato na matumizi.  na hatua aliyochukua Mheshimiwa Thabita ni kupeleka taarifa hizi kwa mkurugenzi  na mkuu wa wilaya kwa hatua zaidi. Lakini pamoja na changa- mwingine alichukua mchanga akatuletea mifuko 15,” anaeleza Mwenyekiti wa sasa wa kijiji cha  Shande, Andrea Lubango.  Kwa hakika wananchi ndio wamiliki wa kiti cha uenyekiti na wanapoamua kuchukua kiti chao wanaweza, kama wana Shenda wangeamua kukaa kimya na kundelea kuhuzunika na kulalamika tu pasipo kuchukua hatua hakuna ambacho kingAewezekana Na watoto wao wangeendelea kusoma kwenye madarasa yenye vumbi kutokana na kutokuwa na sakafu. Hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuweza kuhakikisha Wanashenda wanapata mapato yenye thamani sawa na mchanga uliochanganyika na dhahabu.

No comments:

Powered by Blogger.