PSSSF yawanoa wanahabari Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza kwa lengo la kuwajengea ufahamu wa huduma zinazotolewa na mfuko huo na pia kuimarisha mahusiano.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika Alhamisi Juni 12,2025 yakishirikisha zaidi ya wanahabari 30.
Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, Happness Manyenye amesema mfuko huo umeboresha huduma zake ikiwemo wanachama kujiandikisha na kupata taarifa za mafao yao kidigitali kupitia mfumo wa 'PSSSF Member Portal'.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mahusiano mema baina ya PSSSF na wanahabari na kwamba yataongeza weledi wakati wa kuandika habari na kuelimisha za jamii na watumishi wa umma kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
No comments: