LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la Msichana Tai latoa mafunzo kwa mabinti, wadau kuhusu ufeminia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Msichana Tai limetoa mafunzo kwa wasichana na wadau mbalimbali wa haki za mtoto wa kike ili kuwawezesha kufahamu dhana ya ufeminia (Feminism) unaohimiza utetezi wa haki za mwanamke na vuguvugu la msichana ni tai, siyo kuku.

Mafunzo hayo yamefanyika Alhamisi Juni 12, 2025 Ilemela mkoani Mwanza, yakishirikisha wanafunzi kutoka klabu za Msichana Tai, walimu na wasichana walio nje ya shule.

Kupitia vuguvugu la msichana ni tai, siyo kuku washiriki wamehamasishwa kupinga mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike na kuamini kuwa msichana ana uwezo wa kuruka juu kama tai na siyo kuku anayesubiri kufanyiwa kila kitu.

"Lengo ni kumjengea msichana uthubutu, stadi za maisha na uongozi huku jamii ikihamasishwa kuamini uwezo wake sawa na wa mvulana" amesema Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Msichana Tai, Halima Juma.

Takribani washiriki 40 wamenufaika na mafunzo hayo ya siku mbili kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Lindi na Dar es salaam ambapo wamepitishwa katika historia ya wanawake waliopigania ufeminia kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuwajengea hamasa wasichana.

No comments:

Powered by Blogger.