LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI YA MSALALA YATAKIWA KUWEKA MAWAKALA WA UKUSANYAJI KODI MGODI WA ACACIA BULYANHULU.

Na:Shaban Njia
HALMASHAURI ya Wilaya ya Msalala Mkoani  Shinyanga imetakiwa kuweka mawakala kwa ajili ya ukusanyaji wa  mapato ya Halmashauri hiyo katika Mgodi wa Dhahabu wa Acacia Bulyanhulu  kama chanzo chake cha mapato ya ndani ili kuwa rahisi katika kujua  tozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Mrabaha na Ushuru wa Huduma.

Hayo yalisemwa juzi na madiwani wa Halmashauri hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika Mjini hapa na kuongeza hali hiyo imekuja baada ya kupambanua kwa mapato ya tozo za Mrabaha na Ushuru wa Huduma zinazotololewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu.

Walisema kuwa katika kipindi cha  julai mwaka jana hadi Desemba jumla ya makisio ya kiasi cha shilingi bilioni 1.4 yaliowekwa na Halmashauri hiyo juu ya tozo hizo hayakuweza kufikia kwani kiasi shilingi milioni 916.1 ndio kiliweza kupatikana na hivyo kuwa na tofauti ya kiasi cha shilingi milioni 543.8 sawa na asilimia 63 hakikiweza kupatikana

Mmoja wa Madiwani hao Matilda Msoma kutoka kata ya Ikinda alisema kuwa Mapato kwa ajili ya Ushuru wa Huduma pamoja na Mrabaha yamekuwa yakichanganywa katika taarifa za Halmashauri hiyo na kuongeza kuwa ni bora zikatofautishwa na hivyo kuweza kujua kama kuna tatizo katika sehemu za Mrabaha au Ushuru wa Huduma.

Msoma alisema katika kipindi hicho cha mwaka jana  jumla ya Makampuni 25 yalilipa Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 400 huku kiasi cha shilingi Bilioni moja ikiwa kama Mrabaha kiasi ambacho ni kidogo kulingana na Makampuni yaliopoa katika Mgodi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliwataka Madiwani kuhakikisha kuwa wanayajua makampuni yote yanayofanya kazi katika Mgodi huo wa Bulyanhulu hata kama yapo yanayofanya kazi kwa siku moja nayo yatozwe tozo kama yalivyo mengine.

Kawawa aliendelea kusema kuwa kuna watu wanaoleta bidhaa mbalimbali katika Mgodi huo lakini Halmashauri haiwajui na kuongeza kuwa wamiliki wa Mgodi huo wanawajua na hivyo kuwafumbia macho katika kuhakikisha kuwa wanalipa ushuru kwa Halmashauri husika.

“Kuna baadhi ya Makampuni ambayo yamekuwa yakileta bidhaa mbalimbali katika Mgodi huo lakini Halmashauri ya Msalala haiyajua huku Kampuni ya Acacia ikiwatambua  hali hii inaipotezea halmashauri mapato mablimbali ya ndani kwa ajili ya kuendeshea shughuli za Maendeleo.

Aliwataka Madiwani hao kuhakikisha kuwa wanasimaia mapato yao ya ndani hasa katika eneo hilo la Migodi na kuhaidi kuwa yeye kama Serikali atawaunga mkono katika kuhakikisha kuwa Halmashauri ya Msalala inapata stahiki zake zote kutoka kwa wawekezaji hao hasa wa Migodi.

No comments:

Powered by Blogger.