OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA YANG'AKA KUHUSU KUANDIKWA KWA TAARIFA ZA KIKAO CHA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MWANZA.
Kaimu Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza na Wanahabari hii leo alasiri, ambapo ameonya wanahabari na vyombo vya habari kuacha kuandika habari kuhusiana na Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa wa Mwanza kilichoketi Jumamosi January 15,2016.
Na:Binagi Media Group
Ikumbukwe kuwa ni kikao hicho ndicho kilichosababisha Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Faisal Issa kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kutokea mvutano katika kikao hicho baina yake na mmoja wa Viongozi wakubwa Mkoani Mwanza.
Baada ya kikao hicho, taarifa mbalimbali zimekuwa zikiandikwa katika vyombo tofautitofauti vya habari nchini, hatua ambayo imemlazimu Kaimu Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Willium James kukutana na Wanahabari Jijini Mwanza na kuonya juu ya taarifa hizo kuendelea kuandikwa kwa kuwa ni za upotoshaji na kwamba Kamati hiyo haitarajii kusoma/kusikia katika vyombo vya habari juu ya taarifa alizoziita za upotoshaji kutoka katika kikao hicho cha kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mwanza.
Hii ndiyo taarifa kamili
Kulia ni Kaimu Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Willium James akizungumza na wanahabari alasiri ya leo.
Wanahabari
No comments: