WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA PEPSI JIJINI MWANZA WAGOMA.
Na:Binagi Media Group
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Soda cha
Pepsi kinachomilikiwa na Kampuni ya SBC Tanzania Jijini Mwanza, leo wamegoma
kufanya kazi kiwandani hapo wakishinikiza mwajiri wao kuwaboreshea maslahi yao.
Wafanyakazi
hao ambao wanafanyaka kazi kwa mkataba wa muda mfupi (vibarua), wamedai kuwa
wamefikia hatua hiyo kutokana na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa mwajiri wao
ambae ni Wakala wa ajira katika Kiwanda hicho, Kampuni ya SARAMA Investiment
ambayo hata hivyo wamebainisha kuwa imefutiwa kibali cha kusimamia ajira zao
kiwandandani hapo.
Wamefafanua
kwamba Kampuni ya SARAMA Investment imekuwa ikisimamia ajira zao kinyume cha
sheria za kazi, kwa kuwa jukumu la Kampuni hiyo kiwandani hapo lilikuwa ni
kushughulikia suala la kutafuta wafanyakazi na kwamba suala la malipo
linafanywa na kampuni ya SBC Tanzania tofauti na ilivyo sasa ambapo kampuni
hiyo ya Uwakala wa ajira ndiyo inayoshughulikia malipo yao.
Wamesema
kutokana na hali hiyo, Kampuni ya SARAMA Investment imekuwa ikiwanyima haki zao
ikiwemo kuwalipa malipo kidogo ya shilingi Elfu Sita kwa Kutwa, badala ya
shilingi Elfu Tisa kwa kutwa na kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu jambo
ambalo wamesema hawatakubaliana nalo.
Itakumbukwa
kwamba wiki chache zilizopita, Waziri wa nchi, ofisi yaWaziri Mkuu, Sera, bunge,
ajira, kazi, vijana na walemavu Mhe.Jenista Muhagama, alifanya ziara katika
Kiwanda hicho na kutoa maagizo ya kufuta leseni ya Kampuni inayolalamikiwa na
wafanyakazi hayo ya SARAMA Investiment kwa kukiuka sheria za ajira nchini.
INSERT…………..WAFANYAKAZI
Katika ziara
aliyoifanya katika kiwanda cha Pepsi Jijini Mwanza, Mhe.Muhagama aliagiza ajira
za wakafanyakazi hao kusimamiwa na Kampuni inayomiliki Kiwanda hicho ambayo ni
SBC Tanzania huku akitamka kufuta leseni ya Kampuni ya SARAMA Investment inayolalamikiwa
ambayo bado inasimamia ajira za wafanyakazi hao.
INSERT……………JESTINA MUHAGAMA
Hadi
tunakwenda katika chumba cha habari, mazungumzo ya kutatua mgomo huo yalikuwa
yakiendelea baina ya wawakilishi wa wafanyakazi hao, Viongozi wa Kampuni ya
SARAMA Investment pamoja na afisa ajira Mkoa wa Mwanza ambapo wanahabari
hawakuruhusiwa kuingia katika mazungumzo hayo.
No comments: