LIVE STREAM ADS

Header Ads

IDARA YA MIFUGO BUKOMBE MKOANI GEITA YAINGIA LAWAMANI KWA KUTOA VIBARI VYA KUSAFIRISHA MIFUGO YA WIZI.

NaJoel Maduka, Bukombe.
Wakati wimbi la wizi wa mifugo likiendelea kugonga vichwa bila majibu katika maeneo mbalimbali nchini, wafugaji wa Wilaya ya Bukombe katika Mkoa wa Geita wameitupia lawama Ofisi ya Afisa mifugo Wilayani humo kwa kushindwa kuwadhibiti wasaidizi wake wa Kata ambao wamekuwa wakituhumiwa kutoa nyaraka za serikali kwa wahalifu wanaotuhumiwa kujihusisha na wizi wa mifugo katika Wilaya hiyo.

Mfugaji Thomas Masanja akiwa kwenye yowe (mwano) wa kutafuta ng’ombe 21 zilizoibiwa za mfugaji Vasco Mgwesa, alitoa malalamiko kwa madiwani wa kata za Igulwa, Bulangwa na Iyogelo kuwa amesikitishwa sana na wimbi la wizi wa mifugo kupanda huku akimrushia lawama Ofisa mifugo wilaya Bukombe George Sabuni na maofisa mifugo wake wasaidizi kwa kutoa vibari vya kusafirishia ng’ombe kwenye magari kwenda mikoa ya Tabora na Dar es salaam.

Alisema walishakamata kibari alichotoa ofisa mifugo kata ya Runzewe Mohamed Mwangeni kwa ajili ya kusafirishia ng’ombe za wizi ambapo malalamiko hayo yaliungwa mkono na menyekiti wa wafungaji kanda ya ziwa Juvenary Mulashani wakati akiwa kwenye eneo ambalo limekuwa likitumiwa kupandishia mifugo hiyo kwenye maloli marufu kwa jina la uwanja wandege lililopo katika hifazi ya halmashauri ya Bukombe.

Mulashani alisema niukweli usiopingika nikwamba” tunaushahidi wiki iliyopita tulikamata Ng’ombe 39 zilizokuwa zimeibiwa katika kijiji cha Butubili na kukamatwa mkoai Tabora wezi hao wakiwa na kibali cha serikali kutoka kwa Ofisa mifungo wilaya ya Bukombe.”

Alisema kuwa ng’ombe nyingi zimekuwa zikiibiwa wilaya ya Biharamulo na wilaya zingie kisha kusafilishwa pori kwa pori hadi uwanja wandege na maofisa wa mifungo kwenda huko kwa kutumia magari ya serikali kutoa vibari na wakati mwingine maofisa hao hutoa bibari nayakati za usiku tena kwenye hifadhi ya halmashauri ambako hairuhusiwi gari wala mtu yeyote kuingia bila kibari toka ofisi ya misitu.

Diwani wakata ya Iyogelo Juma Lushiku akiwa kwenye mwano wa wafugaji wakifatilia ng’ombe 21 za Vasco Mgwesa mkazi wa kijiji cha Butubili kata ya Igulwa wilayani hapa zilizo ibiwa februari 4 usiku wa kuamukia Februari 5 ambazo hadisasa hazijapatikana baada ya kupakizwa kwenye gari aina ya Funso na kufaulishwa kwenye lolli nyingine ambalo halijulikani.

Lushiku alisema hali hiyo ya kuibiwa ng’ombe imesha kithiri na imewafanya wafugaji kutokua na amani na mifungo yao hasa nyakati za usiku wanapo ingia kulala alisema.

“ hakika huu ni mda wa kutumbua majibu halimashauri, na kuwachukulia hatua zakinizamu watumishi waliotajwa kuhusika na tuhuma za kutumia madarakayao vibaya kwa kutumia nyaraka za serikali kwa wizi wa ng’ombe ikiwa vitendo vinavyo fanywa na maofisa hao ni kuwaludisha nyuma wafugaji kimaendeleo.”alisema Mh.Lushiku.

Mwenyekiti wa halmashauri Mayala Safari alishtushwa na taarifaa kuwa hifadhi ya Halmashauri kuna uwanja wa ndege wa kuibia ng’ombe  hivyo ikalazimu aungane na madiwani wengine kwenda kuona uwanja huo akiwa eneo hilo aliomba polisi kuwasaidia wafugaji wanapokuwa wameibiwa ng’ombe nakwamba wafugaji waimalishe ulinzi wa sungusungu.

Safari alisema madiwani wamelipokea na wamejipanga kuhakikisha wanakomesha tabia za watumishi wanaotajwa na kwamba walisha fikishwa polisi kuhojiwa kumbe mchezo huo bado unaendelea hivyo amewaomba wafungaji watulie kwani watalifikisha kwenye vikao vya kamati zinazo endelea na maamzi yatatolewa siku ya baraza la madiwani ili kutumbua majipu haya.

Ofisa mifungo wilaya George Sabuni alikiri kupokea kesi ya kufikishwa polisi kesi za baadhi ya wasaidizi wake akiwemo Ofisa mifungo kata ya Runzewe magharibi Mohamed Mwangeni kwamba kunakibari alichokitoa cha kusafilishia ng’ombe mkoani Tabora ambapo ng’ombe hao walikamatwa kuwa mali ya wizi na kwa kuwa swala hilo bado linafanyiwa uchunguzi na polisi ushahidi ukikamilika watakao bainika watachikiliwa hatua za kiutumishi.

No comments:

Powered by Blogger.