LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA MPANGO WA INJILI YA UPONYAJI NCHINI AJITOSA RASMI KUPAMBANA NA MAUAJI YA ALBINO.

Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadau wengine wakifuatilia mashindano ya Miss Albino yaliyofanyika hivi karibuni Jijini Mwanza.
Judith Ferdinand, Mwanza
Mkurugenzi wa Mpango wa Injili ya Uponyaji ambaye pia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Lucy Haruni, anatarajia kufanya tamasha maalumu  kwa ajili ya kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi mapema mwezi Mei mwaka huu, katika wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Akizungumza na BMG alisema,  kupitia  kipaji alichobarikiwa na Mungu cha uimbaji, ataendelea kuhamasisha jamii kuacha kufanya vitendo vya ukatili na  mauaji dhidi ya  watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Haruni alisema, kupitia tamasha hilo ataielimisha jamii kuhusu madhara wanayoyapata walemavu hao wanapo fanyiwa vitendo hivyo ikiwmo ulemavu wa kudumu pamoja na vifo hali inayopelekea taifa kuwa na ongezeko la watu tegemezi.

Pia alisema kupitia huduma ya uimbaji atawasomesha  watoto watano wenye ulemavu kutoka kituo cha  Mitindo kilichopo Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, mpaka  mwisho wa elimu yao.

Alisema ataendele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi sambamba na unyanyapaaa kwa walemavu wa viungo kwa njia ya matamasha kwani mwezi Agousti  mwaka huu, anatarajia kuwa mkoani Tabora kuendeleza kazi hiyo.

Aidha aliiomba serikali na wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kazi zake ili aweze kuendelea kutoa huduma na kuelimisha jamiii kupitia uimbaji, kwani mpaka sasa ameisha kamilisha album  ya kwanza inayokwenda kwa jina la Tembea na Yesu, iliyobeba ujumbe wa kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

No comments:

Powered by Blogger.