LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA WAWAZAZI WENYE WATOTO WA VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI KUZINDUA TAWI MKOANI MWANZA.

Judith Ferdinand na Getruda Ntakije, Mwanza
CHAMA cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa  (vichwa maji) na Mgongo Wazi Tanzania (ASBAHT), wanatarajia kuzindua tawi la chama hicho mkoani hapa.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika  Apili 4 mwaka huu, katika Hospitali ya Rufaa Bugando na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Abdulhakim Bayakub,   viongozi wa chama hicho kutoka Sweden, uongozi wa Bugando na serikali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa Onesmo Rwakendela.

Hayo yalisemwa jana  na Mkurugenzi wa  Shirika la Marafiki wa Watoto wenye Kansa Tanzania (FoCC), Walter Miya, ambalo  ni wadhamini wa chama hicho wakati akizungumza na majira ofisini kwake.

Miya alisema, lengo la umoja huo ni kuwakutanisha wazazi wenye watoto hao, ili waweze kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo suala  la namna ya kukabiliana na  changamoto  za malezi.

“Tunatarajia kufungua tawi la chama  cha wazazi wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi katika hospitali ya Bugando ambao umelenga kuwasaidia wakina mama hao kushirikiana   na kuelimishana juu ya namna watakavyo kabiliana na changamoto za kuwalea watoto hao,” alisema Miya.

Aliongeza kuwa, katika uzinduzi huo uongozi wa chama hicho kutoka Sweden utapata fursa ya kutembelea  wodi ya watoto hao na kuongea na wazazi wao, ili kufahamiana na kujua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika  kuwalea na kuwapatia matibabu.

No comments:

Powered by Blogger.