LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI USHETU ALALAMIKIWA KUWACHONGANISHA MADIWANI NA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Isabela Chilumba ametuhumiwa kuwashitaki Madiwani wa halmashauri ya hiyo,  kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malicela  ya kuwa wamekaidi agizo la kuhamia katika makao makuu ya Halmashauri hiyo.

Mmoja wa Madiwani wa halmashauri ya Ushetu, amesema kuwa kitendo hicho kimelenga kuwachonganisha Madiwani na kiongozi huyo wa juu wa Mkoa na kwamba wao wapo tayari kuhamia makao makuu ya halmashauri hiyo ikiwa miundo mbinu iliyopo itaboreshwa ikiwemo ofisi, upatikanaji wa Maji na sehemu za kufanyia vikao na si Godauni la tumbaku.

Akiongea na wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo pamoja na Madiwani hao katika Kata ya Nyamilangano wiki iliyopita, Mkuu wa Mkoa aliwataka wakuu wa Idara pamoja na Madiwani kuhamia katika makao makuu ya Halmashauri ya Ushetu yaliyoko Nyamilangano lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa wananchi wa Kata hiyo pamoja na Wilaya nzima ya Ushetu.

No comments:

Powered by Blogger.