LIVE STREAM ADS

Header Ads

102.5 LAKE FM MWANZA, WAMTAMBULISHA MENEJA WAO KWA WANANZENGO.

Katika Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, 102.5 Lake Fm ambayo ni radio mpya ya Jijini Mwanza, imemtambulisha Meneja wake kwa Wananzengo (Wananchi).

Katika akaunti za Twitters, Facebook na Instagram za radio hiyo, kuna zoezi la kuwatambulisha wafanyakazi wake ambapo jana kulikuwa na post ikisomeka; "Wananzengo wenzetu wa 102.5 Lake Fm Mwanza, Kutana na Mwananzengo na Meneja wetu aitwae Jenipher Deus.
Raha Yake Ya Rock City ni Kula Mihogo Ya Kuchemshwa.
NAWE TUAMBIE RAHA YAKO YA ROCK CITY NI NINI?
Ungana nasi Facebook, Twitter & Instagram @lakefmmwanza
#102.5LakeFmMwanza
‪#‎RahaYaRockCity
‪#‎RadioYaWananzengo

Hata hivyo radio hiyo bado iko kwenye matangazo ya majaribio yaliyoanza Machi 14 mwaka huu, lakini imepokelewa vyema Jijini Mwanza ambapo sasa kila mmoja anatamani kujua ujio wake utakuwa vipi, hususani katika vipindi vyake ili kuendana na kauli mbiu yake kuwa yenyewe ni "Raha Ya Rock City".

No comments:

Powered by Blogger.