LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA KUUNGURUMA KATIKA MKUTANO WA HADHARA HII LEO JIJINI MWANZA.

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM Taifa), Shaka Hamdu Shaka, hii leo anatarajiwa kuunguruma Jijini Mwanza, katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Katibu UVCCM Wilaya ya Ilemela, Comred Kheri James ,ameiambia Binagi Blog-BMG, kwamba kabla ya mkutano huo, Shaka anakutana na Makatibu Wakuu wa UVCCM kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kikao cha utendaji cha ndani.

"Katibu Mkuu UVCCM Taifa anafanya ziara ya Kikazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa. Leo atakuwa na Mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Magomeni ambapo kabla ya mkutano huo atakutana kwanza na Makatibu wa UVCCM kutoka Mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera na Mwanza". Amesema James na kuongeza;

"Lengo la Mkutano huo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kutekeleza ilani yake, pili ni kuwahamasisha wananchi kufanya kazi na tatu ni kuwahamasisha vijana kutumia fursa zilizopo na pia kujua ni fursa zipi hizo ili kutengeneza uchumi imara kwa taifa". Amefafanua.

Amewahimiza wananchi wote kwa umoja wao kuhudhuria mkutano huo kwa kuwa utakuwa mkutano wa aina yake, ambapo mkutano huo utakaanza majira ya saa nane mchana, huku pia ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM.
Katibu UVCCM Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, Comred Kheri James.

No comments:

Powered by Blogger.