LIVE STREAM ADS

Header Ads

JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KUTUMBUA MAJIPU ZAUNGWA MKONO.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umesema utaendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli juu ya yale yote anayoyatekeleza ikiwemo kuwachukulia hatua viongozi wasio waadilifu maarufu kama utumbuaji wa majipu.

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Mwanza, katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Magomeni Kirumba.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shama akihutubia katika Mkutano wa hadhara Jijini Mwanza hii leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano huo. Amekemea vitendo vya rushwa kwa baadhi ya viongozi Mkoani Mwanza na kusema kuwa chama kitaendelea kuwabaini wala rushwa na kuwatumbua.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ilemela, Comred Kheri James akihutubia katika Mkutano huo.
Ametomwomba Katibu Mkuu UVCCM Taifa, kufikisha kwa rais kilio cha wakazi wa Jiji la Mwanza kunyanyaswa na wawekezaji wenye viwanda. Pia ameomba ahadi ya Rais Magufuli ya kutoa Milioni 50 kwa kila Mitaa na Vijiji itimizwe kwa wakati na kuwanufaisha kwanza vijana na Wanawake.
Katibu wa UVCCM Taifa, pia akigawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM wapatao 100.
Katibu wa UVCCM Taifa, pia akigawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM wapatao 100.
WaCCM pamoja na Wananchi wakifuatilia kwa Umakini Mkutano huo
WaCCM pamoja na Wananchi wakifuatilia kwa Umakini Mkutano huo
WaCCM pamoja na Wananchi wakifuatilia kwa Umakini Mkutano huo
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa (katikati) akifurahia jambo na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Pata Habari Zaidi HAPA

No comments:

Powered by Blogger.