ALICHO KISEMA DOGO RICHIE KUHUSU MUZIKI WAKE NA BARAKA DA PRINCE.
Moja kati ya wasanii wa muziki wa
kizazi kipya wenye muziki mzuri ni pamoja na Dogo Richie a.k.a "Richie
Ree" ingawa bado kunawatu hawaja mtambua vizuri muziki wake.
Baada ya
kuisikiliza na kuitazama video ya wimbo wake mpya "Yoyoba" na kupitia
nyimbo zake kadhaa Super News Tz team iliamua kumfuatilia na kutaka kujua life
style yake ya Muziki ipoje, baada ya kumpata msanii huyo alilazimika kufunguka
na kusema.
“Kwa majina naitwa Francis Kazungu
Kalama Jina la sanaa Dogo Richie a.ka Richie Ree, Baba yangu ni Mkenya Mama
yangu ni Mtanzania mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto 6, nilianza
muziki 2013 Studio yangu ya kwanza kuingia ilikuwa ni ‘Jungle Masters’ chini ya
Producer ‘Emmy D’ ambaye ndiye Producer wangu hadi sasa.
Hadi kufikia sasa nina jumla ya nyimbo
4 na Collabo moja Naona raha, Sina raha, Yoyobah, Hayana Mjuzi & So nice
ft. Sam Wa Ukweli. ‘Naona raha’ ni moja kati nyimbo zilizo nitambulisha vizuri,
Muziki katika maisha yangu ndio kila kitu no muziki hakuna kinachoweza kwenda
ingawa kupitia muziki nimeweza kuanzisha biashara zangu ndogo ndogo ambazo
pindi napo kuwa sina Show zinakuwa zinanisaidia kuendesha maisha.
Baraka Da Prince ni msanii ninaye
mfagilia sana Tanzania, coz anamuziki mzuri, Changamoto kwenye muziki zipo ila
kikubwa ambacho nakiona kwangu ni ‘Marketing’ ya muziki wangu ili uweze kufika
mbali zaidi, coz malengo yangu ni makubwa yaani ni kufika level za kimataifa.
Mwisho nimshukuru mwenyezi Mungu, Fans
wangu na wadau wote wanao endelea kunipa support kwenye Muziki maana wao ndio
maisha yangu Thanks”.
No comments: