BENKI YA CRDB YAOMBWA KUWAJALI WANAHISA WAKE.
Na:Shaban Njia
Wanahisa wa Benki ya CRDB Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, wameiomba benki hiyo kuwawezesha kifedha ili kuhudhuria vikao mbalimbali vya kitaifa vinavyoandaliwa na taasisi hiyo badala ya wao kujitegemea.
“Kwa sasa Wanahisa tunajigharamia wenyewe katika vikao hali ambayo kwa sisi Wanahisa inakuwa ni vigumu kuhudhuria vikao kutokana na kukosa fedha na hivyo kupelekea kutopata elimu ya kutosha katika fani ya biashara kwa ujumla”. Walisema wanahisa hao katika kikao baina yao benki ya CRDB mjini Kahama.

No comments: