LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYANI MWANGA CHAKIRI KUPITIA WAKATI MGUMU.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akikabidhi Kadi za chama kwa wanachama wapya baada ya kufungua Shina la Vijana Wakereketwa wajasiriamali Kilang'wa Wilayani Mwanga.
Na:Fahadi Siraji
Pamoja na kukiri kupitia siasa za majitaka wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Chama Cha Mpinduzi CCM Wilaya ya Mwanga Mkoa kilimanjaro kimesema bado wanachama wake ni imara na wamoja na kwamba wasiokubali kuyumbishwa kisiasa.

Hayo yalisemwa jana  na Katibu wa CCM  Wilayani humo, Mwanaidi Hussein Misha, wakati akitoa neno la  shukran mara baada ya Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka  Hamdu Shaka kuzungumza na viongozi wa vijiji, kata pamoja na wanachama wa chama hicho katika Wilaya hiyo.

"CCM iliioachwa na marehemu baba Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Abeid Karume, Mzee Rashid Kawawa na Mzee Thabit Kombo itabaki kuwa kimbilio na tarajio la wananchi wengi katika kufanikisha masuala yao ikiwemo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Alisema Misha na kuongeza;

"Shaka nimekuwa nikikusikiasikia tu katika vyombo vya habari, wewe bado ni kijana mdogo ila unatosha kubeba hata dhamana kubwa, endelea Mungu atakusaidia ili uthibitishwe kuwa Katibu Mkuu kwa kuwa uwezo unao wa kukitumikia vyema  kiti hicho" Aliongeza Mbisha.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa kilimanjaro, Juma Raibu Juma, aliisifu Wilaya ya Mwanga kwa kuendelea kuwatoa mchanga wa macho kwa kulinda jimbo hilo lisichukuliwe na upinzani.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, anaendelea na ziara yake Mkoani Kilimanjaro na baadae ataelekea katika Mikoa ya Tanga

Wanachama wapya wakila kiapo cha Chama
Mti wa kumbukumbu mara baada ya kuwasiri katika ofisi ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro
Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wanachama wa CCM  Mapema Wilayani Mwanga
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akikabidhi Mpira kwa kiongozi wa Timu ya soka ya vijana wa CCM Wilayani Mwanga
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka, akikadhi Jezi kwa Captain wa Timu ya Kileo juu
Mkuu wa Utawala, Omary Mwanang'walu akisalimia wananchi Wilayani Mwanga
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Kirimanjaro Juma Raibu akizungumza katika Mkutano wa Hadhara
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akihutubia wananchi katika mkutano wa Hadhara Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kirimanjaro.

No comments:

Powered by Blogger.