LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA ACACIA BUZWAGI YABANWA NA KAMATI YA BUNGE.

Na:Shaban Njia
Kampuni ya Acacia inayaomiliki Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, juzi ilijikuta ikibanwa na Kamati ya Ukimwi ya Bunge kuhusu kuhusu baadhi ya wafanyakazi wake kuachishwa kazi baada ya kubainika kuwa na Maambukizi ya Ukimwi.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbuge wa Jimbo la Singida Mjini, King Elbarick, alisema suala kama hilo haliwezi kufumbiwa macho na kuongeza kuwa ni lazima serikali ichunguze hali halizi ili kubaini undani wa suala hilo na kuchukua hatua mara moja.

Nae Mbunge kutoka katika Jimbo la Tarime Vijijini John Heche alisema kuwa Kampuni kama ya Acacia lazima isadie Wagonjwa walioathirika na Ukimwi waliolazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, kwa kutoa huduma kama vile chakula.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Costantine Kanyasu, aliunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa mgodi huo unapaswa kuhakikisha kuwa unatoa misaada ya lishe kwa wafanyakazi wake hususani wenye maambukizi ya Ukimwi.

Awali Mratibu wa Magonjwa ya Ukimwi kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Henry Sylivester, alisema changamoto kubwa inayowakabili Wagonjwa wa Ukimwi ni ukosefu wa lishe bora licha ya mashirika mbalimbali kujitokea kwa hali na mali katika kusaidia suala zima la chakula kwa wenye maambukizi ya Ukimwi.

No comments:

Powered by Blogger.