LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC MWANZA AHOFIA ONGEZEKO LA WATUMISHI HEWA. AJA NA MKAKATI MADHUBUTI.

Judith Ferdinand na Getruda Ntakije, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,  amesema baada ya siku kumi ataunda timu kutoka Mkoani, itakayofanya kazi katika Halmashauri zote Mkoani Mwanza kwa ajili ya kuhakiki watumishi.

Timu hiyo itafanya kazi kwa siku 7 ndani ya halmashauri zote , kwa ajili ya kubaini watumishi hewa, hii ikiwa imetokana na mkoa   wa Mwanza kutwajwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa ya kuwa na watumishi hewa.

Mongella alitoa kauli hiyo jana katika kikao baina yake na Waandishi wa Habari, kilichokuwa na dhumuni la kujitambulisha kwao.

"Baada ya siku kumi, nitaunda timu kutoka mkoani, itakayofanya kazi ya uhakiki watumishi ndani ya siku saba katika halmashauri zote, hivyo  kila mtumishi atatakiwa kufika  na picha ndogo mbili, pia wataweka sahihi za vidole vyao, na kwa wale ambao wako likizo na masomoni wanatakiwa kuwasili maeneo yao ya kazi kwa ajili ya zoezi hilo". Alisema Mongella.

Aliongeza kuwa ana wasiwasi baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, kuna uwezekano mkubwa kwamba idadi watumishi hewa Mkoani Mwanza itaongezeka zaidi ikilingalishwa na idadi ya watumishi hewa 334 waliobainika hapo awali.

No comments:

Powered by Blogger.