LIVE STREAM ADS

Header Ads

LEMBELI KUCHUKUA MAAMUZI YAFUATAYO BAADA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI SHAURI LAKE.

Na:Shaban Njia
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga jana imetupilia mbali shauri la kutenguliwa matokeo ya Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kahama Mjini, lilifunguliwa aliekuwa mgombea wa kiti  hicho kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) James Lembeli dhidi ya Mpinzani wake Jumanne Kishimba ambaye anaongoza Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Katika kesi hiyo nambari 1/2015 iliyokuwa ikiendeshwa na Jaji Moses Mzuna iliyofunguliwa na James Lembeli katika Mahakama Kuu ya Shinyanga Mwezi Novemba mwaka jana ilikuwa ikimtuhumu Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Juamnne Kishimba kwa kutoa Rushwa katika Kampeni zake Ubunge, kutotendewa haki na msimamizi wa Uchanguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Akitoa hukumu hiyo katika Mahakama kuu Kanda ya Shinyanga iliyofanyika katika Wilaya ya Kahama Jaji Moses Mzuna alisema kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini hayawezi kutenguliwa kutoka na Ushahidi wa upande wa mleta maombi James Lembeli kutojitosheleza.

Akizungumza na Wananchi pamoja na  Wanachama wa Chadema muda mfupi baada ya kutoka Mahakamani, Lembeli aliwataka Wananchi kuwa watulivu kwani kitendo kilichofanywa na Mahakanama hiyo sio cha haki na kuongeza kuwa atakaa na Mwanasheria wake Mpale Mpoki ili kuliangalia upya suala hilo na kuangalia jinsi ya kufanya.

No comments:

Powered by Blogger.