LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBUNGE KIGOMA KUSINI AKABIDHI MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO WILAYANI UVINZA.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Mbunge wa Jimbo la kigoma Kusini, Hasna Mwilima (CCM), amekabidhi msaada wa shilingi milioni sita na laki tatu, na tani kumi na saba za vyakula kwa wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Kironda kata ya Sunuka Wilayani Uvinza , yaliyotokea februari 13 mwaka huu na kusababisha maafa makubwa.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji hicho wakati akikabidhi misaada hiyo iliyotolewa na Halmashauri ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma na wadau mbalimbali alisema  serikali kwa kuwathamini wananchi imeamua kutoa misaada ilikuweza kuwasaidia wahanga waliopoteza vitu vyao wakati wa mafuliko.

Mwilima aliupongeza uongozi wa Mkoa wa kigoma na halmashauri zote kwa kutoa msaada wa vyakula tani saba zitakazo wasaidia waadhirika hao kupata chakula  katika kipindi hiki ambacho wanajipanga kurekebisha makazi yao.

Pia aliishukuru Halmashauri ya Uvinza kwa kuthamini Wananchi wake na kutoa msaada wa shilingi milioni tano na Mwenyekiti wa Halmashauli hiyo kuongezea laki mbili na kwamba hiyo inaonyesha ni jinsi gani serikali ya awamu ya tano inavyo wathamini wananchi.

"mimi kama mbunge wenu nitatoa shilingi milioni moja, nitaongezea katika mchango wa Viongozi wengine waliotoa na tutahakikisha tunashirikiana wakati waraha, wakati washida na nyakati zote tutakuwa pamoja na nitawahudumia ipasavyo ndugu zangu". alisema Hasna.

Kwa upande wake kaimu Mkuruge wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza,Bernad Lusomyo alisema kamati ya maafa ilifika kijijini hapo na kufanya utathimini wa maafa na kubaini kumetokea uharibifu wa zaidi  ya shilingi milioni 35 na Halmashauri imeweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano.

Alisema fedha hizo zimetolewa iliziweze kuwasaidia wahanga Serikali haiwezi kulipa pesa zote hizo zilizo fanyiwa utathimini amewaoma wananchi kuwa wavumilivu na kulizika na kidogo walicho kipata serikali inapenda sana kuwasaidia.

Hata hivyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuchangia Chakula tani saba kupitia michango iliyotolewa na Halmashauri zote za Mkoa ilikuweza kuwasaidia Wanakijiji waliokumbwa na mafuriko.

Rehema Hassani ni mmoja kati ya Wahanga wa mafuriko pia ni Mkazi wa Kironda alisema kwaniaba yawanakijiji wenzake wanaishukuru Serikali pamoja na  Mbunge kwa kutoa misaada hiyo tunaimani itatusaidia na tutaweza kujipanga upya na kuziendesha familia zetu.

Aliiomba Serikali kuwapatia maeneo mengine waweze kujenga na kuondoka kuishi mabondeni ambapo mvua kubwa ikinyesha maji nanajaa mtoni na kuingia ndani kupelekea mafuliko hivyo serikali igawe maeneo mengine yakuweka makazi.

Msaada uliotolewa ni maharage kilo 218, mchele kilo1,240 unga, mihogo, mahindi na mafuta ya kupikia na chumvi ambapo shilingi milioni sita na laki tatu watakazo gawiwa wahanga wa mafuriko hayo zilitolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali.

Pia Mbunge huyo alikabidhi mashuka 218 kwa Halmashauri  ya uvinza yaliyotolewa na Bohari ya Dawa MSD yaliyonunuliwa kutokana na pesa za bajeti ya mtoto wa Afrika ambayo iliahirishwa ili bajeti hiyo isaidie shughuli za kijamii.

No comments:

Powered by Blogger.