LIVE STREAM ADS

Header Ads

KISHIMBA ALALAMIKIA HUDUMA ZA AFYA MBELE YA WAZIRI MWENYE DHAMANA.

Na Shaban Njia, Kahama
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba juzi amelalamikia kitendo cha Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kuwaandikia Wagonjwa kwenda kupima vipimo vya mionzi katika Hospitali Binafsi kwa gharama kubwa mara mbili badala ya ile iliyopangwa katika Hosptali za Serikali.

Kishimba alitoa malalamiko hayo mbele ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia watoto na wazee, Mh.Ummy Mwalimu, alipotemblea Hospitali hiyo kujinea changamoto zinazowakabili wagonjwa wanaopata matibabu katika Hospitali hiyo.

Alisema kuwa Watumishi katika Hospitali hiyo wamekuwa na tabia ya kuwaandikia Wangonjwa vipimo vya mionzi kwenda kupima katika Hospitali za binafsi kwa gharama kubwa ya shilingi 45,000 kwa mtu mmoja badala ya shilingi 7,000 iliyopangwa katika hospitali za Serikali.

Waziri Mwalimu aliutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha kuwa unatengeneza mfumo mzuri wa Wananchi kutoa malalamiko yao katika uongozi wa Hospitali hali ambayo itasaidia katika kupunguza kero zao badala ya kwenda kulalamika katika ngazi za juu za uongozi.

No comments:

Powered by Blogger.