RAIS MAGUFULI APONGEZWA.
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamanoro Mashariki Manispaa yaMkoani Mwanza, Trasisius Kabuche ampongeza Rais Magufuli, kwa hatua aliyochukua ya kuelekeza fedha za sherehe ya Muungano inayoadhimishwa kila mwaka Apili 26, kutumika katika ujenzi wa barabara kuanzia Nera mpaka uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Kabuche amesema, hatua aliyochukua Dkt.Magufuli ni ya kizalendo, kwani anaonyesha alivyo na uchungu na maendeleo ya nchi.
Aliongeza kuwa , ni jambo jema kwa maendeleo ya taifa kwani kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha, zinazotumika katika maadhimisho ya sherehehe mbalimbali huku wananchi wakikosa huduma muhimu za kijamii.
Pia alisema, wananchi wamekuwa na kilio cha muda mrefu juu ya kupata kiongozi ambaye yuko tayari kutetea maslahi ya taifa na kuleta maendeleo kwa jitihada na juhudi binanfsi.
Hata hivyo alimuomba Dkt.Magufuli kutoishai katika sherehe za Muungano, ila aangalie na suala la mbio za Mwenge ambao unagharimu fedha za wananchi , na badala yake fedha hizo hazielekeze katika sekta ya elimu, afya na ajira kwa vijana.
Aidha aliongeza kwa kumuomba Dkt.Magufuli kusimamia suala la katiba kwa ustawi wa maendeleo ya taifa kwa vizazi vijavyo, kwani hili nchi iendelee kukua kiuchumi inaitaji mfumo ambao kila kiongozi atatakiwa kufuata kutokana na utawala kubadilika badilika huku kiongozi kwa wakati huo kuongoza atakavyo.
Wakati huo huo aliwaomba, wananchi na viongozi mbalimbali kumuuunga mkono rais, kwa kila mtu kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kiutendaji, ili kuleta maendeleo ya taifa na kuacha kutegemea msaada kutoka kwa wafadhili wa nje.
No comments: