LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA MAFUNDI UJENZI 90 WANUFAIKA NA KAMPUNI YA MABATI YA ALAF JIJINI MWANZA.

Mhandisi wa Kampuni ya utengenezaji Mabati ya ALAF, Daudi Kidyamali, akitoa maelezo  kwa mafundi ujenzi  waliotembelea kiwanda Kampuni hiyo Jijini Mwanza, kabla ya mafunzo ya semina ya kuelimishwa mafundi hao juu ya utumiaji wa vifaa bora vya ujenzi.
Judith Ferdinand, Mwanza
Mafundi ujenzi 94 Jijini Mwanza wamenufaika na semina ya mafunzo ya namna ya  kutumia bidhaa bora  za kuezekea  zinazozalishwa nchini ili kukuza uchumi wa taifa.

Semina hiyo iliandaliwa na kampuni ya kutengeneza mabati ya ALAF, ililenga kuwaelimisha, kuwaelekeza na kuwakutanisha pamoja kwa ajili ya kufahamiana  ili kuweza   kubadilishana ujuzi.

Meneja wa Kampuni ya ALAF Tawi la Mwanza Sourav Roy, amesema wamekuwa wakitoa mafunzo kama hayo kila mwaka kwa ajili ya kuwaelimisha mafundi namna ya kujua bidhaa nzuri zitakazoboresha shughuli zao.

mmoja wa mafundi waliohudhuria semina hiyo, Adelfinus Mwijage, ameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa mafunzo hayo, kwani yatawajenga, nakuleta mshikamano baina yao, na pia kuwasaidia kuboresha kazi zao.

No comments:

Powered by Blogger.