LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA ALIVYOHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI MONDULI MKOANI ARUSHA.

Baada ya kuwasili katika Wilaya Ya Monduli Mkoani Arusha, Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (wa tatu kulia) alianza kufanya shughuli za kijamii kwa kupanda mpunga katika Mashamba ya UHANDENI Wilayani humo. 

Hiyo ilikuwa miongoni mwa shughuli za kijamii alizoshiriki katika ziara yake ya kikazi ya siku tano iliyohitimishwa juzi aliyoifanya katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Mbali na shughuli hizo, pia alihutubia katika mkutano wa hadhara.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Akinawa baada ya kutoka shambani
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akizungumza na viongozi wa chama na Jumuiya mara baada ya kutoka Shambani.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka alipanda mti katika ofisi ya ccm kata ya Selela kama Kumbukumbu

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka alipokelewa na wananchi wa kijiji cha Serela kwa shwange na nderemo.

Katika Mkutano wa hadhara, wazee wa kijiji cha serela walimzindika kama ishara ya kumpokea katika kijiji hicho.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (kushoto) akimsimika Ukamanda, Peter john Bega katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akisalimia wananchi wake na kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka kuzungumza katika Mkutano wa hadhara

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akihutubia wananchi wa kijiji cha Serela Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akihutubia wananchi wa kijiji cha Serela Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara
Kwa umakini, Kumsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, akiwaaga wananchi wa Monduli Mkoani Arusha na kuelekea Mkoa wa Manyara kuanza ziara nyingine ya Kikazi.
Picha na Fahad Siraji.

No comments:

Powered by Blogger.