LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHALALAMIKIWA KUTUMIA RUSHWA UCHAGUZI MDOGO MKOANI KIGOMA.

Kwa Ushonaji wa Nguo Nzuri, wasiliana nasi 0688 44 74 44 or 0767 68 38 88 tuko Ghana Green Vie Jijini Mwanza.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Chama cha ACT Wazalendo, kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa marudio wa kumchagua Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagunga mkoani Kigoma huku ushindi huo ukigubikwa na tuhuma za rushwa kutoka kwa baadhi ya wananchi.

Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya aliekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho kwa tiketi ya CCM, kushindwa katika rufaa iliyokatwa dhidi yake na mgombea wa ACT Wazalendo.

Akitangaza matokeo katika ushaguzi huo wa marudio, msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kijiji cha Kagunga, Regina Mgande, alimtangaza  Mikidadi kutoka ACT Wazalendo kuwa mshindi kwa kura 1,337 akifuatiwa na mgombea wa CCM  aliepata kura 1,274 ambapo kura 27 ziliharibika.

Mbali na ushindi huo, chama cha ACT Wazalendo kimelalamikiwa na baadhi ya wananchi kuwa kilitumia rushwa ya chumvi kuwashawishi wapiga kura na hatimae kuibuka na ushindi huo.

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho, wamesema wananchi wengi wamemchagua mwenyekiti huyo baada ya kushawishiwa kwa mifuko wa chumvi ambayo ilitolewa na baadhi ya viongozi wa ACT Wazalendo.

Juhudi za kuwatafuta viongozi wa ACT Wazalendo kuzungumzia tuhuma hizo bado zinaendelea.

No comments:

Powered by Blogger.