LIVE STREAM ADS

Header Ads

JEMBEKA FESTIVAL 2016, MAPOKEZI YA MSANII NEYO JIJINI MWANZA NI NOMA.

Neyo check out from the hotel Hyatt Regency
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo jana akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016. Kulia ni Meneja wa Hoteli hiyo, Timothy Mlay.

Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jana jioni akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.

Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza leo katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.
Attu Mynah and Neyo
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Neyo ta Hyatt Regency-The Kilimanjaro
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Neyo official car Mercedes Benz GLE 350 D of 2016
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Neyo Sorrounded by Tanzanian Bodyguard
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Neyo at Julius Nyerere International Airport
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza jana jioni.
Neyo arrived in Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua jijini Mwanza. 
Sebastian Ndege
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja.
Neyo on Maasai Shuka
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza jana jioni.
Getrude Clement na Neyo
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-show love na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. 
Neyo playing with a snake in Mwanza
Waooooo, Michezo ya kuchezea nyoka kutoka Bujora
IMG_5305
Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Sebastian Ndege na Neyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza leo katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Imeandaliwa na Zainul Maige

No comments:

Powered by Blogger.