LIVE STREAM ADS

Header Ads

MBAO FC YA JIJINI MWANZA KUANZA KUKISUKA KIKOSI CHAKE CHA MAANGAMIZI LIGI KUU MSIMU UJAO.

AfricanLyon

Klabu ya soka ya Mbao FC ya jijini Mwanza, imetangaza kuanza usajili wa wachezaji wake watakaoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ujao kuanzia wiki ijayo.

Wakati timu hiyo ikijiandaa na usajili huo, BMG imepata taarifa za ndani kutoka katika klabu hiyo inayomilikiwa na wafanyabiashara wa mbao wenye makazi yao Manispaa ya Ilemela, zinasema kwamba usajili huo utaanza baada ya kocha wa timu hiyo kuwasili rasmi.

Kumbuka timu ya Mbao FC imepanda ligi kuu ikitokea ligi daraja la kwanza baada ya kufuzu kwa bahati nasibu kutokana na klabu za Geita Gold ya mkoani Geita, Jkt Oljoro ya mkoani Arusha na Kanembwa FC ya mkoani Tabora kushushwa daraja kutokana na kubainika kujihusisha katika sakata la upangaji matokeo.

Katibu Mkuu wa Mbao FC, Richard Atanas, alisema klabu hiyo inajua ni wapi itawatoa wachezaji wake lengo likiwa ni kukisuka kikosi cha timu hiyo ili kujiweka sawa katika mapambano ya ligi kuu msimu ujao.

No comments:

Powered by Blogger.