UTALII WA NDANI WAZIDI KUPATA MASHIKO.

Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi.
Na Dickson Mulashani
Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamasika na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana katika mbuga hiyo.
Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao, Emmanuel Kalenzi, amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho” alisema.

Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater

Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake
Simba dume akiwa anaunguruma.
Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi
Wanafunzi wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro.
Picha zaidi Bonyeza HAPA
No comments: