LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAKOMAA NA JIJI ILI KUJIPATIA KIPATO.

Baadhi ya wakazi wa Jijini Mwanza wakiwa katika barabara ya Maktaba ya Mkoa wa Mwanza jirani na jengo la Tanesco, wakifanya mahemezi yao.
Licha ya kwamba biashara ndogondogo katika maeneo yasiyo rasmi katikati ya jiji la Mwanza zimepigwa marufuku, lakini wajasiriamali wanakomaa na jiji ili kuhakikisha wanajipatia kipato halali.

Wajasiriamali hawa wameiambia BMG "bado kuna uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara jijini Mwanza hivyo ni muda mwafaka viongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza kuendelea kuainisha maeneo mengi zaidi ili tuweze kufanya shughuli zetu vizuri".

No comments:

Powered by Blogger.