LIVE STREAM ADS

Header Ads

MALARIA BADO NI CHANGAMOTO MKOANI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Dkt.Saula Beichumila (kushoto) ambaye ni mratibu wa udhibiti malaria mkoani Mwanza, akizungumza na Vesterjtz (kulia) katika Uzinduzi wa Mpango wa Ugawaji wa Vyandarua vyenye dawa kupitia Kliniki ya Wajawazito na  Mtoto uliofanyika leo katika Uwanja wa MTC Nyegezi Kona Jijini Mwanza.
Na Vesterjtz wa BMG
Imeelezwa kwamba takribani silimia 23 ya wagonjwa waliofika katika  vituo vya afya kwa kipindi cha miezi sita mkoani Mwanza, wamebainika kuugua ugonjwa wa malaria.

Akizungumza leo katika uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa Vyandarua kupitia Kliniki ya wajawazito na kliniki ya Mtoto, mratibu wa udhibiti malaria mkoani Mwanza Dkt.Saula Beichumila, amesema kuwa takwimu hizo ni za kuanzia kipindi cha mwezi januari hadi mwezi june mwaka huu.

Dkt.Beichumila aliwataka wananchi kuzingatia magizo na miongozo ya wataalamu wa Afya ili kudhibiti kasi na mĂ ambukizi mapya ya ugonjwa huo.

"Zaidi ya wagonjwa wa nje laki nane waliofika katika vituo vya Afya kwa kipindi cha mwezi janury hadi june  asilimia 23 ya wagonjwa hao walibainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria".Alisema Dk Beichumila na kuongeza;

"Hali ya ugonjwa wa malaria kwa mkoa wa Mwanza bado ni kubwa hivyo niwaombe wananchi kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa Afya ili kutokomeza ugonjwa huo".

Alisema zipo iman potofu kwamba vyandarua hivyo vinavyogawiwa bure kwa akina mama wajawazito vinaharibu nguvu za kiume na kuwataka kupuuza uzushi huo kwani si wa kweli.

No comments:

Powered by Blogger.