LIVE STREAM ADS

Header Ads

UZINDUZI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA USAFI KWA MACHINGA JIJINI MWANZA WAGUBIKWA NA DOSARI YA UBADHIRIFU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza-SHIUMA, Matondo Masanja, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) vyenye thamani ya Shilingi Laki Sita, kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi. Hafla hiyo imeambatana na Kauli Mbiu isemayo "Machinga Kukaa Katika Mazingira Safi Inawezekana, Tusonge Mbele Kwa Usafi".
Na BMG
Shughuli ya kukabidhi vifaa vya usafi vilivyotolewa na Shirika la Machinga mkoani Mwanza SHIUMA imeingia dosari baada Mwenyekiti wa Shirika hilo kutofautiana kauli na Katibu wake, juu ya matumizi ya fedha za mkopo zilizotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Hayo yamejili baada ya kusomwa kwa risala ya machinga katika shughuli hiyo iliyofanyika katika eneo la Makoroboi, bila kuainisha kwamba SHIUMA pia ni miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mikopo midogo midogo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Hali hiyo ilisababisha diwani wa Kata ya Nyamagana na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha, kuhoji ni kwa nini SHIUMA haikuweka bayana kwamba ilipokea mkopo wa Shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, hali iliyosababisha machinga kupiga kelele kwa madai kwamba uongozi wa SHIUMA kutumia mkopo huo bila kuwanufaisha wanachama wengine.

Alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, Katibu wa SHIUMA,Venatus Anatory, alikiri uongozi kupokea mkopo wa shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kwamba Shilingi Laki Sita kati ya fedha hizo, zilitumika kununua vifaa vya usafi vilivyokabidhiwa jana huku Mwenyekiti wa Shiuma,Matondo Masanja, akisema fedha za mkopo bado zipo na kwamba baadhi ya wanachama watanufaika na fedha hizo kwa njia ya mkopo.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, amewaagiza viongozi wa Shiuma kuhakikisha fedha hizo za mkopo zinakopeshwa kwa wanachama na si kufanya manunuzi ya vifaa vya usafi kama Katibu alivyoeleza na kwamba viongozi hao wahakikishe wanaweka wazi mapato na matumizi ya fedha za wanachama.

Vifaa vilivyotolewa na wamachinga hao ni pamoja na madumu 20 ya plastic ya kuwekea taka na mifagio 20 itakayotumika kufanya usafi ambapo wamachinga hao wamesema lengo lao ni kutoa vifaa kwa maeneo yote ya jiji la Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza, Matondo Masanja.
Diwani wa Kata ya Nyamagana na Kaimu Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (kushoto), akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Katibu wa SHIUMA, Venatus Anatory, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Ombeni Mbise (katikati) akisoma risala ya machinga Jijini Mwanza kwa niaba ya Katibu wa SHIUMA, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, Mkoa wa Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Francis Sisamo ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Nasoro Hemed ambae ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamagana Magharibi Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Makoroboi Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Edmund Kaiza ambae ni Meneja wa Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi mkoani Mwanza, akifafanua namna kituo hicho kilivyojipanga kuwasaidia Machinga Jijini Mwanza kujikomboa kiuchumi ikiwemo utayari wake wa kujenga Soko Kubwa kwa ajili ya Machinga (Machinga Complex) katika eneo la Makoroboi Jijini Mwanza ikiwa mamlaka husika zitakubaliana na wazo hilo ambalo limeidhinishwa na Machinga.
Baadhi ya Machinga Jijini Mwanza wakifuatilia kwa ukaribu hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya, diaba kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya, diaba kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), Diwani wa Kata ya Nyamagana na Kaimu Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (katikati), wakimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya (kulia), fagio kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.