LIVE STREAM ADS

Header Ads

SALAMU ZA SHUKURANI KUTOKA BARMEDAS TV MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kufuatia kifo cha mkuu wa vipindi ktk kituo chetu cha barmedas.tv Mwl.Charles Sokoro (pichani), tunapenda kutoa shukrani Wanahabari binafsi,  Vyombo Vyao vyao, Vyama vya MPC na UTPC Kwa ushirikiano mlioutoa katika Kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu.

Hatutoweza kumshukuru Mtu mmoja mmoja kwa sababu  tunaamini mchango wa kila mmoja ulikuwa mkubwa na tunauthamini.
Imetolewa na 
Simba Kabonga - Msemaji barmedas.tv
Kwa Niaba ya barmedas MEDIA 

Nami nikiwa kiongozi mwandamizi wa kampuni hii nichukue frusa hii kuwashukuru ndg zangu wanahabari wenzetu, Kwa nguvu mlizo ziongeza juu ya mzee wetu.

Hii imeonyesha kuwa tupo pamoja pia na ushikiano katika matatizo kama siyo kwenye fraha tu, Niwaombe tu twendelee kuishi kwa upendo tusamehane pale tulipo kwazana, Kwa kuwa thamani ya Msamaha ni Makosa.

Kiukweli hatuna cha kuongea kwenu kwa kile mlicho kionyesha hata kwa kutushika mkono, Mungu awabariki sana na hili liendelee hata kwa wengine lisikomee leo,

Imeandikwa upo wakati wa kuzaliwa lkn pia upo wakati wa kufa, Hili hatutalikwepa kwa maana moja tu, Maneno haya yamethibitishwa kitabu cha Isaya Mungu anasema,
Neno limtokalo kinywani mwake kamwe halitarudi bure.

Asante BMG members wote kwa kutuheshimu Mungu awazidishie pale mlipo toa kwa kuwa mmetoa kwa moyo lkn mmepanda mbegu njema hata kwa Mungu wenu, Mungu Awajalie hata ambao hamkufika lkn pia hata ambao mmeenda Musoma kwenye msiba poleni tupo pamoja twendelee kuombeana, kama yupo nitayake mkwaza naomba msamaha pia nipo tayari kujifunze.
Jey Kapongo
Marketing Manager btv

No comments:

Powered by Blogger.