LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYABIASHARA WA SARUJI MKOANI SHINYANGA WATAKIWA KUPANUA WIGO WA BIASHARA ZAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Shaban Njia, Kahama
Wafanyabiashara wa Saruji mkoani Shinyanga, wametakiwa kupanua wigo wa biashara zao badala ya kuwekeza katika sehemu moja hali inayoweza  kupelekea kuyumba kwa mitaji yao kutokana na kuwa na mzigo mwingi katika maghala yao.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Saruji ya Simba Cement Kanda ya Ziwa, Justice Kanju, aliyasema hayo juzi katika kikao kilichofanyika Kahama mkoani Shinyana kikiwa na lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara wa simenti juu ya muungano wa Kampuni ya simu ya Vodacom na Kampuni ya Saruji ya Simba Cement ili weweze kulipia mizigo wanayoagiza kwa kutumia M-pesa bila ya kuwa na makato yeyote.

“Ninawashauri wafanyabiashara wa Kahama kupanua wigo wa Biashara zenu, kama upo hapa jaribu kuangalia na maeneo mengine kwa hapa nchini bado kuna masoko mengi mapya ya kufanyia biashara na msijirundike katika sehemu moja”. Alisema Kanjua.

Kwa upande wake Meneja Biashara na Masoko M-pesa kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania, Mercy Siyovelwa, alisema kuwa lengo la kuungana kwa Kampuni yake na Kampuni ya Saruji ya Simba ni kuwafanya wateja wake kutumia njia hiyo ya M-pesa katika kuagiza mizigo yao katika kiwanda chao pamoja na mawakala wao waliopo sehemu mbalimbali hapa nchini.

Nae Wakala wa Kampuni ya Saruji ya Simba Cement wilayani Kahama, Ahmed Gulamrasuly, alisema huduma liyoanzisha kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya Simba italeta changamto hasa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwani msongamano wa malipo utapungua na kwamba hata malipo yao katika kuagiza mizigo yatakuwa yakilipwa kwa wakati.

No comments:

Powered by Blogger.