LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYABIASHARA WA PEMBEJEO ZA KILIMO KANDA YA ZIWA WAPEWA SEMINA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo ikiwemo viuatilifu kutoka mikoa   ya Mwanza, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora, Mara, Singida, Pwani na Kigoma, wamepatiwa mafunzo  yatakayowasaidia kuwaelimisha na kuwaelekeza wateja wao ambao ni wakulima.

Hayo yalibainishwa jana na Ofisa Mfawidhi Kitengo cha Huduma ya Afya ya Mimea Mwanza, Doroth Lusheshanija, katika  mafunzo ya taaluma maalum ya viuatilifu, yaliyoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu Katika Kanda za Kitropiki (TPRI)Arusha, yanayoendelea mkoani hapa.

Lusheshanija alisema, mafunzo hayo yapo kisheria, kwani sheria ya  udhibiti wa visumbufu ya mimea ya mwaka 1997 na kanuni zake za mwaka 1999, inamtaka mfanyabiashara wa viuatilifu kuwa na taaluma hiyo.

Pia alisema, itawasaidia wafanyabiashara kujua sheria na kuacha kuuza bidhaa hizo ambazo hazijasajiliwa na kuisha muda wa matumizi sambamba na kutatua changamoto ya wakulima kulalamika juu ya viuatilifu.

Aidha alisema, washiriki wengi hawajajitojeza kushiriki, hivyo  mafunzo hayo ni endelevu kutokana na uhitaji uliopo kwa sasa kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo.

Naye Mratibu wa Mfunzo  hayo kutoka (TPRI) Arusha Habib Mkalanga alisema, wanataka nchi iendelee kwa kilimo, hivyo itakuwa sahihi kwa wafanyabiashara na wakulima kupata elimu itakayosaidia kuhakikisha wananyunyuzia  viuatilifu kwa wakati, ili kupata mazao mengi na salama.

Vile vile alisema, kupitia mafunzo hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuwaelekeza kwa usahihi wateja wao, hii ni kutokana na maelekezo yauchanganyaji wa viuatilifu  yanayowekwa juu ya vifungashio kuwa tatizo kwa wakulima.
Kadhalika aliziomba halmashauri kuhimiza Ofisa Ugani, kushiriki katika mafunzo kama hayo ili kupata elimu ya ziada ambayo watatumia kuelimisha wakulima wao njia sahihi.

No comments:

Powered by Blogger.