LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAIKUWA KAZI RAHISI CCM KUSHINDA UCHAGUZI MKUU-UVCCM NYAMAGANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na BMG, Mwanza
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Odilia Abraham Batimayo (pichani), amesema haikuwa kazi rahisi CCM kushinda uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Nyamagana kutokana na ushindani uliokuwepo.

Pia ameongeza kazi ilikuwa ngumu katika kushinda nafasi ya urais ikizingatiwa kwamba wakati CCM ilipokuwa ikihakikisha kwamba inatetea kiti chake, pia upinzani ulikuwa ukihakikisha kwamba unachukua kiti hicho.

"Haikuwa kazi rahisi kurejesha jimbo la Nyamagana (lililokuwa chini ya Chadema),nguvu, hekima na ushawishi vilitumika sana. Kumshawishi mtu mpaka akuelewe si kazi rahisi hivyo tunamshukuru Mungu tuliweza kushinda". Amesema Batimayo wakati akizungumza leo asubuhi katika kipindi cha Pambazuko kinachorushwa na redio Metro Fm ya Jijini Mwanza.

Aidha Batimayo amewatupia lawama viongozi wa Chadema kwamba wanatafuta kiki kwa kumuita Rais majina ya ajabu huku wakitumia oparesheni zenye uchochezi kama Ukuta na kwamba wao hawakubaliani na oparesheni hiyo.

"Toka lini Tanzania ikawa na udikiteta tena. Neno hili niliweke kama neno la uchokozi, ni methali inayotaka kuleta uchokozi, kama ni mikutano na vikao kila mtu akafanye jimboni kwake". Amesema Batimayo na kuongeza;

"Tutakapo kuwa watulivu na kumuacha rais akafanya kazi zake ikiwemo kujenga viwanda tutapa ajira, tuache masuala ya kuandamana, tuwaunge mkono viungozi wetu ili kuendana na kasi ya rais ya hapa kazi tu, pia tuunge mkono kauli ya rais ya kutokaa vijiweni, na tutumie fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi badala ya kutumia viroba na kwenda kwenye ukuta ambao hatijui hata utaishia wapi".

No comments:

Powered by Blogger.