IDADI YA WATALI WA NDANI YAONGEZEKA KWENYE HIFADHI YA KISIWA CHA SAANANE JIJINI MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Picha Kutoka Maktaba ya BMG ikionesha mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza akiruka juu katika eneo la "Jumping Point" kwenye Kisiwa cha Saanane.
Na James Salvatory, BMG Dar es salaam
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2011 - 2016 hifadhi ya kisiwa cha Saanane, idadi ya watalii wa ndani imekuwa ikiongezeka na kwa mwaka 2015 /16 watalii wa ndani ilikuwa 94.5% ya watalii wote.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mh.Ramo Makani, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam na kuongeza kwamba ongezeko hilo limepelekea mapato kuongezeka kutoka Tsh.17,796,250 mwaka 2011/12 hadi kufikia tsh. 162,353,610 kwa mwaka 2015/16.
Katika miaka hiyo mchango wa mapato kutokana na watalii wa ndani ni 56% ukilinganisha na 44% ya watalii wa nje huku hifadhi ya Ngorongoro kwa miaka mitano 2010 - 2014 watalii wa ndani waliongezeka kwa wastani wa 12.1%.
Aidha Waziri Makani alisema wizara ya Mali asili na Utalii imejipanga kukuza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu,kuhifadhi vivutio na mazingira yake,kuboresha utalii wa ndani,kuendeleza vivutio vilivyopo na kuanzisha vipya kama (beach tourism and marine tourism),kuboresha utoaji huduma yaani semina na mafunzo mbalimbali na mwisho kuboresha utangazaji wa vivutio.
Kwa hatua nyingine Naibu waziri alisema kumekuwepo na uanzishaji wa hoteli kiholela na kwa sasa wamejipanga kwenda kutekeleza sheria kwa maana ya kuisimamia sheria ya utalii ya mwaka 2006 kwa ukaguzi kwani wamiliki wengi wa hoteli waamesajiri hoteli zao tofauti na huduma wanazotoa.
Naye mkurugezi wa Wizara ya Mali asili na Utalii Zahoro Kamaga alitolea ufafanuzi kuhusiana na huduma za maradhi yaani nyumba za wageni (lodge ,hoteli na moteli) ambapo alisema“MOTEL ni aina ya hoteli iliyojengwa kwenye barabara kuu (High way) na nilazima Moteli iwe karibu na petron station.
LODGE ni huduma ya kulala wageni ambayo iko kwenye vivutio vya kitalii na ni kosa kuita lodge kwenye miji na badala yake unatakiwa uite town hotel hivi vigezo tutaviweka kwenye tovuti yetu ili watu wajue vigezo hivyo.”
No comments: