LIVE STREAM ADS

Header Ads

MARUFUKU KUTUMIA VITUO VYA MABASI YA MWENDO KASI KAMA VYOO-RC MAKONDA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Picha kutoka Maktaba ya BMG
Na james salvatory- Dar es salaam (BMG)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda,
amewataka wafanyabiashara ndogondogo (machinga), kuondoa biashara zao kwenye barabara  za mabasi ya mwendo kasi ili kutohatarisha usalama wao huku pia akionya vituo vya mabasi kutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu ya vyoo (kujisaidia).

Makonda amesema hivi karibuni amepata malalamiko kutoka katika uongozi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka DART kuwa kumekuwa na wafanyabiashara wadogowadogo huyatumia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mabasi hayo kama  vyoo na kupanga biashara zao kwenye barababara hizo hali inayosababisha usumbufu.

''Hivi karibuni nimepokea malalamiko kutoka kwenye uongozi wa DART ya kuwa kumekuwa na baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo wakitumia vituo hivi vya mabasi yaendayo haraka DART kama sehemu ya vyoo  na kuweka biashara zao''amesema Makonda .

Amesema nilazima wafanyabishara hao kufuata utaratibu na misingi ya sheria ikiwemo kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira na kufuata kanuni za mipango miji kama ilivyokusudiwa .

''Hakuna haki pasipo kutenda haki hivyo ninawataka wafanyabishara kuzingatia kanuni za usafi kwani hivi karubuni tunao mpango wakujenga miundombinu ikiwemo ya vyoo katika
vituo vya mwendokasi.

Kuwepo kwa wafanya biashara wadogo wadogo katikati ya mji kumekuja baada ya agizo la Raisi  John Maguli, kuwaruhusu wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao bila kubugudhiwa wakati serikali ikijipanga kuwatafutia maeneo rasmi ya kufanya shughuli zao.

No comments:

Powered by Blogger.