MBOWE AELEZA SABABU ZA MAANDAMANO YA UKUTA KUPIGWA TAREHE.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Baraza kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, limeahirisha Maandamano ya kupinga kile walichokiita Ukuta yaliyokuwa na dhana ya Umoja wa Kupinga Udikiteta Tanzania yaliyokuwa
yamepangwa kufanyika kesho Septemba Mosi kote nchini.

Akitangaza uamuzi huo leo, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, amesema baraza
limefikia uamuzi huo baada ya kuombwa na viongozi wa dini ili kutoa fursa kwa viongozi hao kuendelea
kutafuta muafaka dhidi yao na serikali.
Hata hivyo Mbowe amesema maandamano hayo yatafanyika kama yalivyopangwa Oktoba Mosi mwaka huu kama hakuna maridhiano yatakayopatikana licha ya kwamba awali yaliishazuiliwa na jeshi la polisi nchini.
Imeandaliwa na BMG kwa msaada wa Mtandao.
No comments: