LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATUMISHI WA SERIKALI NCHINI WATAKIWA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZA WATUMISHI HOUSING.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for KISESA WATUMISHI HOUSINGNa James  Salvatory - BMG Dar
Watumishi wa Taasisi za Umma nchini, wameshauriwa kununua nyumba ambazo zimeshajengwa tayari kuliko kununua viwanja kwani ujenzi wa nyumba huchukua muda mrefu ikiwemo kutumia gharama nyingi wakati wa ujenzi.

Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Watumishi Housing (WHC) Fred Msemwa, juzi aliwaambiwa wanahabari kwamba viwanja vingi nchini havijapimwa na ujenzi wa nyumba  nyingi Tanzania umekuwa ukichukua miaka miwili hadi mitano huku ukiambatana na kuibiwa vifaa vya ujenzi wakati wa ujenzi na hivyo kujengewa nyumba zisizokuwa na viwango wakati huo ukiwa unalipa kodi muda wote wa ujenzi.

Alisema kwa upande wao kama Watumishi Housing wamekuwa wakiuza nyumba kwa bei tofauti kwa lengo la kukidhi mahitaji ya kila mmoja kwani nyumba zao wanauza  shilingi milioni 27 hadi milioni 76 kulinga na nyumba yenyewe.

Aidha Msemwa aliunga mkono uamuzi wa serikali kuhamishia makao makuu yake mjini Dodoma na kwamba hiyo itawapa nafasi wao kama WHC, kunufaika katika sekta ya ujenzi kwa kuongeza ajira kuchochea uwekezaji na ukuaji wa viwanda vinavyohusiana na mambo ya ujenzi pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa kodi na mapato mbalimbali ya serikali na hata mikoa ya jirani itanufaika pia.

No comments:

Powered by Blogger.