LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI ATAKA MWAFAKA DHIDI YA ZUIO LA MAANDAMANO NA MIKUTANO YA KISIASA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatotory
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji  Francis Mutungi, amevitaka vyama ambavyo vinampango wa kuandamana  na kufanya mikutano ya hadhara, kutokufanyaka  hivyo na badala yake vikae katika meza ya mazungumzuko ili kutafuta mwafaka wa zuio la mikutano na maandamano nchini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Jijini dar es salaam, Mutungi alisema  kwenye Taifa lolote lile kama kuna kuwa na sintofahamu, njia sahihi ya kuitatua ni mazungumzo na kuwaomba wadau wenye mpango wa mikutano na maadamano wasubiri kwanza na watumie mazungumzo kuleta mwafaka.

Aidha Jaji Mutungi aliwatoa hofu wananchi  kuhusu taharuki ya uvunjifu wa amani ambayo imejengeka miongoni mwao kutokana na kauli za maandamano zilizotangazwa na wanasiasa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.