LIVE STREAM ADS

Header Ads

STAA WIZKID KUTOKA NIGERIA KUUNGANA NA MASTAA WA BONGO KUDONDOSHA BURUDANI YA TIGO FIESTA 2016 JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Agost 20,2016 ule msimu wa burudani Tanzania, Tigo Fiesta 2016, unaanza rasmi ambapo show ya kwanza inapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha shilingi elfu kumi (10,000).

Mastaa kibao kutoka Tanzania, wakiwemo Niki wa Pili, Fid Q, Ben Pol, Joh Makini, Aika na Nareel, Dayna Nyange, Mr.Blue, Man Fongo na Ommy Dimpoz, wanakutana kwenye jukwaa moja la Tigo Fiesta 2016 na msanii Wizkid kutoka Nigeria ili kuufungua msimu huo wa burudani nchini.

Picha imepigwa kwenye mkutano na waandishi wa habari (Press Conference), uliofanyika leo kwa kuwahusisha pia waandaaji wa Tigo Fiesta pamoja na wasanii watakaotoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza.
Na BMG
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Tigo Fiesta 2016, Sebastian Maganga (mwenye kinasa sauti), akizungumza kuhusiana na maandalizi ya kukamilika kwa show hiyo kabla ya kumkaribisha msanii Wizkid (wa tatu kulia) kutoka Nigeria ili kuzungumzia show hiyo.
Wizkid akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari (Press Conference) kuhusu Tigo Fiesta 2016 Jijini Mwanza ambapo amesema amejiandaa vyema kudondosha burudani kali kwenye show hiyo.
Elias Mwenda kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza, akiuliza swali kwenye mkutano wa waandishi wa habari, kuhusu Tigo Fiesta 2016 uliyofanyika Jijini Mwanza leo.
Msanii Wizkid kutoka nchini Nigeria (wa nne kulia waliokaa) akiwa na baadhi ya wasanii kutoka Tanzania watakaopiga show ya kwanza ya Tigo Fiesta 2016 hii leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Miongoni mwa wasanii hao ni Niki wa Pili, Fid Q, Ben Pol, Joh Makini, Aika na Nareel, Dayna Nyange, Mr.Blue, Man Fongo na Ommy Dimpoz.
Tazama HAPA Fiesta ya Mwaka 2014 Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.