LIVE STREAM ADS

Header Ads

SUMATRA YAZUIA WAMILIKI WA MABASI YA MIKOANI KUSITISHA HUDUMA YA USAFIRI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvantory, BMG Dar
Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu majini (SUMATRA), imewaagiza wamiliki wote wa mabasi ya masafa marefu kuendelea kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria hadi hapo utaratibu wa ukaguzi utakapotolewa tena.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Gillard Ngewe, amesema kutokana na taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari kuhusu huduma ya usafiri kutokuwepo siku ya tarehe 22 Agosti 2016 (jumatatu), Sumatra inafuatilia jambo hilo na kuhakikisha huduma ya usafiri kwa abiria inakuwepo wakati wote.

Aidha amesema pamoja na nia njema ya TABOA ya kutaka zoezi la ukaguzi kufanyika, Sumatra imewaagiza wamiliki wote wa mabasi ya masafa marefu (mabasi ya mikoani), kuzingatia masharti ya leseni ya usafirishaji ikiwemo kuendelea kutoa huduma ya usafiri kwa abiria hadi hapo utaratibu wa ukaguzi utakapotolewa tena.

Kwa upande mwingine mkurugezi huyo amepongeza maadhimio makuu matatu ya TABOA  ambayo ni kufunga vifaa kuratibu mwendo kwenye mabasi yao (Vehicle tracking system), kutangazia umma rasmi kuwa wameamua kwa kauli moja mabasi yao yote kutembea mwendo wa kilometa 80 kwa saa na mwisho kwanzia tarehe 22/8/2016 mabasi yote yatakakaguliwa na kupewa stika maalum pamoja na madereva wao kutahiniwa ili kutambua umahili wao.

No comments:

Powered by Blogger.