LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU ZA ALLIANCE SPORTS ZA JIJINI MWANZA ZATAKIWA KUNYAKUA UBINGWA KWENYE MASHINDANO YA SHULE ZA SEKONDARI AFRIKA MASHARI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu za Alliance Sports Academy zimepata nafasi ya kupeperusha bendera ya Tanzania katika Mashindano ya Shule  za Sekondari kwa nchi  za Afrika Mashariki na Kati(FEASSA), yanayotarajia kutimua vumbu agousti 24 hadi semptemba 4 mwaka huu, nchini Kenya.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Alliance Sport Academy ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire, katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi bendera wachezaji wa  timu hizo, iliyofanyika wilayani Nyamagana mkoani hapa.
Bwire alisema, kituo hicho kimetoa timu mbili za wavulana na wasichana watakao shiriki katika mashindano hayo na zote ziko kundi B.

Pia alisema, anaamini timu hizo zitafanya vizuri na kurudi na ushindi, kwani timu ya wavulana imejipanga  kwa kufanya mazoezi ya kutosha na wasichana nao wamekaa kambini mwaka mzima na nimara ya kwanza kushiriki.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha aliyemwakilisha Mkuu wa  Mkoa John Mongella katika hafla hiyo alisema, wachezaji wa timu zote mbili wakacheze kwa bidii na kuzingatia yale yote waliofundishwa na walimu wao, na kuipeperusha vyema nchi ya Tanzania, mkoa wa Mwanza sambamba na Jiji la Mwanza kwa  kuhakikisha wanarudi na ushindi.

Pia alisema, wilaya ya Nyamagana ipo tayari kuwaunga mkono ili waendelee kuonyesha vipaji vyao mpaka ngazi ya dunia sambamba na kumpongeza Mkurugenzi wa timu hizo  kuwalea vijana hao kimichezo na kupelekea kupata mualiko wa kushiriki mashindano hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba aliwataka wachezaji hao kuhakikisha wanarudi na ushindi kwa zaidi ya watanzania milioni 49, wanawaangalia wao na wanahitaji furaha kwa kuipeperusha vyema bendera ya taifa.
Hata hivyo Msemaji wa timu hizo Jackson Mwafulango alisema, wanaenda kuwaonyesha Kenya kuwa Alliance inafanya vizuri na wamejipanga kurudi na ushindi.

Nahodha wa  timu ya Alliance Sports Club Hance Masoud  alisema, matarajio yao ni kufanya vizuri na kurudi na ushindi licha ya mwaka jana kushika nafasi ya pili, kwani benchi la ufundi limejipanga na kuwafundisha mbinu mbalimbali.

Aidha Nahodha wa  timu wa Alliance Queens Fc Enikia Kasong alisema, wanaenda ugenini  ila wamejipanga kurudi na ushindi licha ya kwamba wanaweza kukutana na changamoto wanaamini watazikabili kwani wanahitaji kuzingatia nidhamu.

No comments:

Powered by Blogger.