TFF YAOMBWA KUSAIDIA UPATIKANAJI WA SOKO LA MIPIRA YA MIGUU ITAKAYOKUWA IKIZALISHWA NA WAJASIRIAMALI NCHINI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeombwa kusaidia upatikanaji wa soko la mipira itakayokuwa ikizalishwa na wajasiriamali hapa nchini.
Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella katika ufungaji wa mafunzo ya utengenezaji wa mipira ya miguu kwa wajasiriamali wadogo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAN TRADE) na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) tawi la Mwanza, yaliyofanyika chuoni hapo wilayani Ilemela mkoani hapa.
Mongella alisema, TFF ihakikishe inayafahamisha Mashirikisho mama yaliyomo ndani EAC, ili tukishajenga uwezo wa kutengeneza mipira kwa wingi tuwe na uhakika wa soko la ndani na ukanda jambo litakalosaidia kukuza uchumi na michezo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAN TRADE Edwin Rutageruka aliiomba TFF kufanya utafiti wa mahitaji ya mipira hapa nchini, kwani utawaongoza kujua uhitaji wa soko na hivyo kuwaandaa wajasiriamali nchi mzima kutengeneza na kuuza.
"Naomba TFF mfanye utafiti wa mahitaji ya mipira hapa nchini, kwani utatuongoza kujua mahitajj ya soko na hivyo kuwaandaa wajasiriamali wetu nchi nzima kutengeneza na kuuza," alisema Rutageruka.
Pia aliiomba TFF kuanza kufanya kampeni rasmi ya kununua mipira inayotengenezwa nchini sambamba na Mkuu wa Mkoa kutoa maelekezo kwa shule za msingi na sekondari kuanzia januari 2017 kuanza kununua mipira ya miguu kutoka kwa wazalishaji hao, kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya michezo. katika taifa.
Naye Rais wa TFF Jamal Malinzi aliwahakikishia soko la uhakika wajasiriamali hao, kwani kwa mwaka shirikisho linaagiza mipira laki tano kwa mwaka kutoka nje, kwa ajili ya shule za msingi, sekondari na ligi mbalimbali nchini.
Hata hivyo aliwaomba wajasiriamali hao, kuunda umoja ili wakifanya kazi na TFF waweze kupata mipira kwa urahisi na yenye kiwango kinachokubalika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) sambamba na kuwa na chapa yao inayotambulika.

No comments: