LIVE STREAM ADS

Header Ads

TRA YAZINDUA RASMI ZOEZI LA UHAKIKI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA MLIPA KODI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James salvatory –BMG Dar es salaam
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  imezindua rasm zoezi la uhakiki na uboreshaji wa taarifa za usajili  wa namba ya utambulisho wa  mlipakodi yaani (TIN NUMBER).

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini dar es salaam  kamishishina mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania( TRA) ndugu Alphayo Kidata, alisema zoezi hili  litamtaka kila mwenye namba ya m ya utambulisho wa mlipakodi kufika mwenyewe bila kuwakilishwa katIka ofisi za mamlaka kama walivyoainisha kwenye matangazo yao na ofisi zote za mamlaka zimeandaa utaratibu maalum wa kufanikisha zoezI hili.

 Aidha alisema  uzinduzi wa mfumo huu utahusisha mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani na litadumu kwa kipindi cha miezi miwili hadi tarehe 15-10-2016 na tarehe ya kuanza zoezi kwa mikoa ya nje ya dar es salaam itatangazwa baadae.

“Madhumuni ya zoezi hili ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa  kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa tekinolojia,kuwa na idadi  sahihi ya walipa  kodi wake wanaostahili kuwepo kwenye wigo wa kodi.

“kuwaondoa walipa kodi hewa na wale ambao wamekuwa hawajihusishi na  biashara kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na kufungwa kwa kampuni na kuboresha huduma za ulipaji wa kodi na hivyo kuongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji  wa kodi kwa kiwango cha juu na mwisho kuwezesha gharama za ulipaji wa kodi uwe wa nafuu na hivyo kuwawezesha walipa kodi wetu kutimiza majukumu yao ya ulipaji kodi kwa hiari (Tax compliance),’’ alisema Kidata

Aliongeza kuwa  katika mkoa wa dar es salaam kutakuwa na vituo maalum kwa ajiri ya uhakiki wa taarifa kinondoni itakuwa jingo la LAPF-kijitonyama na kibo compelex Tegeta, ilala ofisi ya shauri moyo  na jingo la 14Rays Gerezani na kwa temeke itakuwa uwanja wa taifa.

No comments:

Powered by Blogger.