LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA AFYA AWATAKA MAAFISA USTAWI WA JAMII NCHINI KUHAKIKISHA HAKI YA MTOTO WA KIKE INALINDWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Na James Salvatory – Dar BMG
Maafisa usitawi wa jamii kote inchini watakiwa kuhakikisha haki za watoto zinalindwa hususani zile zinazohusu watoto wa kike.

Hayo yalisemwa juzi ijumaa na Waziri wa Afya, maendeo ya jamii ,jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, katika uzinduzi wa mradi wa kukusanya nguvu ya pamoja kulinda haki za wasichana mkoa wa Mara awamu ya pili, ambapo amewaangiza maafisa usitawi wote wa jamii  katika ngazi ya mkoa,wilaya  na kata kuhakikisha wale wote wanao wapa  watoto wa shule mimba na wanaowaozesha  au kuoza wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za sheria haraka iwezekananvyo.

Alisema sheria za kuwalinda watoto zipo kinachotakiwa ni utekelezaji na kuiomba jamii kuendelea kupiga vita aina zote za unyanyasaji,ukatili na uzalilishaji unaofanywa kwa motto wa kike.

“Mimi msisitizo nauweka kwa wazazi  na walezi wote kuhakikisha tunawapeleka watoto wetu shule bila kubagua wa kike au wa kiume na wanajamii tuhakikishe tunakuwa na mikakati thabiti ya kukomesha mimba za utotoni kwani jambo hili litawezesha kwa kuboresha mazingira,malezi na ulinzi wa watoto ndani ya familia na hata nje ya familia,”Alisema Waziri Mwalimu.

Aidha waziri alisema awamu hii ya pili itazidi kuongeza na kuendeleza mafanikio katika kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa kulenga  wasichana na vijana,viongozi katika jamii na watu maarufu  katika jamii,wataalam na watoa huduma ,vyombo vya habari na watunga sera pamoja na watoa maamuzi na kuunganisha juhudi zao ili kupata ufumbuzi  wa jinsi gani tutaweza kupambana na aina zote za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana hasa wale wanaoishi vijijini.

“wasichana na wanawake wanakuwa na uhuru zaidi wa kiuchumi  (vipato kuboreshwa kuweza kudhibiti rasilimali na kipato, wasichana na wanawake kuwa na uwezo wa kudai haki yao ya kuwa huru kutokana  na mila potofu kama ndoa za utotoni, ukeketaji  na ukatili wa kijinsia  na jamii kufahamu zaidi kuhusiana na haki za wasichana  na wanawake  na kuwalinda kikamililifu dhidi ya ukeketaji ,ndoa za utotoni  na ukatili wa kijinsia,” alisema Ummy.

Kwa upande wake mkurugezi mtendaji wa TAMWA,  Edda Sanga, alisema wao bado wanaangalia kauli ya serikali ili mtoto wa kike anawekezwa katika elimu kwa kupeleka sheria ambayo itajikita kwenye Mahakama ya juu ili mtu asijeweza kukata rufaa.

Naye mkurugezi wa shirika la utu wa mtoto Koshuma Mtegeti alisema katika utafiti wao katika matendo ya kingono yanaonyesha katika watoto watano wawili wanakuwa wameolewa chini ya umri wa miaka 18 na kwa upande wa ukeketaji kwenye watoto kumi unakuta watoto watatu wamekeketwa na inategemeana na mkoa wenyewe maana kuna mikoa idadi huwa inaongezeka.
Tazama Picha Zaidi HAPA

No comments:

Powered by Blogger.