LIVE STREAM ADS

Header Ads

KANISA LA KIMATAIFA LA METHODIST KUJENGA CHUO KIKUU KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mratibu wa Maendeleo Endelevu wa Kanisa la Kimataifa la Methodist duniani, Mchungaji Eric Soard, akizungumza jana kwenye uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha kanisa hilo cha Wesley, katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Na BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dk. Leonard Masale, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Wesley cha Kanisa la Kimataifa la Methodist katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Baadhi ya waliojitokeza kushuhudia zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Wesley cha Kanisa la Kimataifa la Methodist katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Kanisa la Kimataifa la Methodist, limepanga kutumia dola za Kimarekani ambazo ni sawa na zaidi ya sh. bilioni 40, kwa ajili ya kujenga Chuo Kikuu katika Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Maendeleo Endelevu wa kanisa hilo lililoanzishwa mwaka 1990 na kuenea duniani kote, Mchungaji Eric Soard, chuo hicho kitakachoanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka 2017 kitakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 2,500 baada ya kukamilika kwake.

Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa chuo hicho kiitwacho Wesley. Mgeni rasmi aliyeweka Jiwe la Msingi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk. Leonard Masale.

No comments:

Powered by Blogger.