LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE NCHINI ATAKA KILIMANJARO QUEENS KUUNGWA MKONO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Rais wa Chama cha Mpira wa Wanawake nchini (TWFA) Amina Karuma (kulia), akizungumza wakati wa mapokezi ya timu ya soka la Wanawake ilipowasili Jijini Mwanza ikitokea nchini Uganda kwenye michuano ya CECAFA ambapo iliibuka na ubingwa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza.

Judith Ferdinand, Mwanza
Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Wanawake nchini, Amina Karuma, ameiomba Serikali kuunga mkono juhudi za kuinua soka la wanawake.

Karuma alitoa ombi hilo jana Jijini Mwanza wakati wa mapokezi ya timu ya Taifa ya Wanawake Kilimanjaro Queens ikitokea nchini Uganda kwenye michuano ya Kombe la Challenge CECAFA ambayo iliibuka na ubingwa kwa kuilaza timu ya Kenya kwenye mchezo wao wa fainali.

Karuma alisema timu hiyo imeonesha mfano bora baada ya kurudi na ushindi huo hivyo ni jukumu la Serikali na wadau mbalimbali wa soka ikiwemo makampuni kushirikiana na timu hiyo ili kufikisha mpira huo mbali zaidi kwenye viwango vya soka la wanawake duniani.

''Wanawake tumejaribu na tumeshinda, kwa hatua hiyo serikali sasa itutambue na sisi wanawake kwa kutupa nguvu kama ambavyo nguvu kubwa inawekwa kwa wanaume. Alisema Karuma.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitoa pongezi  kwa viongozi wa soka ngazi ya mkoa wa Mwanza na Taifa kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuhakikisha wanarudi na ushindi.

''Mmefanya kazi kubwa ya kuhakikisha mnarudi na ushindi na nitakuwa pamoja na ninyi  ili kuhakikisha mnasonga mbele na kufanya vizuri zaidi katika michuano mingine ijayo. Alisema Mongella.
Kikosi cha Timu ya Soka ya Wanawake nchini, Kilimanjaro Queens, kikiwa Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.